
Washiriki
wanaowania taji la Redds Miss Mwanza 2013, wameanza tambo na majigambo
ya kunyakua Taji hilo, huku kila mmoja akieleza sifa za kushinda taji
hilo.
Wakiongea
kwa nyakati Tofauti wanyange hao walioweka kambi katika Hotel ya New
Mwanza, wamesema mwaka huu pamoja na uwepo wa ushindani katika baadhi ya
mikoa hapa nchini, lakini mkoa wa Mwanza umeonekana kuwa na warembo
wenye ushindani zaidi kufuatia kila mrembo kuwa na vigezo vinavyo
stahili, kupelekea kushindwa kutabili nani atabeba taji la Redds Miss
Mwanza 2013.
Baadhi ya
warembo wamefunguka zaidi na kusema, mikoa ya kanda ya ziwa inayoleta
warembo wao katika Kanda mkoani Mwanza, wajipange zaidi kwani Mwaka huu,
Taji la kanda litabaki Mwanza na hata taji la Miss Tanzania litarejea
Mwanza, kwani historia inaonyesha mkoa wa Mwanza ndio wenye Historia ya
kuchukua Taji la Miss Tanzania mara mbili Mfululizo, ambapo Mwaka 2008
alilichukua Nasreem Karim na mwaka 2009 Miriam Gerald akalichukua tena.
Jumla ya
warembo 14 watapanda jukwaani katika ukumbi wa Yatch Club Mwanza siku ya
Ijumaa ya terehe 14/06/2013 kuanzia saa 2 usiku.
Warembo
hao ni pamoja na Catherine Steven (21), Rose Peter (22), Victoria Newton
(22), Clara Henry (20), Everlyn Charles (22), Esta Perfect (19), Edna
Celestine (18), Judith Josephat (20), Lucy Charles (23), Nasra Muna
(20), Suzan Ikombe (20), Khadija Suddy (20), Angel Lawrence (22), na
Hajra Mohammed (22).


Post a Comment