Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Peter
pinda akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi kitabu cha “Sumbawanga
Ng’ara” kilichoandikwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya
(wa katikati) katika ukumbi wa Dodoma Hoteli Mjini Dodoma, kulia ni
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Sabas Katepa. Kitabu hicho
kinaelezea na kutoa muongozo juu ya usafi na uhifadhi wa mazingira
katika Manispaa ya Sumbawanga, Mkoa wa Rukwa na taifa kwa ujumla. Kitabu
hicho kinauzwa Tsh. 3,500 kwa lengo la kukusanya fedha ya kuchapisha
machapisho mengine zaidi.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Peter
pinda akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho alitoa wito
kwa Uongozi wa Mkoa wa Rukwa kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa
mpango waliouanzisha wa Sumbawanga Ng’ara kwa kuweka mikakati na
kutengeneza sheria ndogondogo za kusimamia mpango huo.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akisoma hotuba yake ya
kumkaribisha Waziri Mkuu kuzindua kitabu cha Sumbawnga Ng’ara ambapo
alimshuru kiongozi huyo Mkuu katika nchi kwa kutenga muda wake pamoja na
waliohudhuria katika hafla hiyo fupi ya uzinduzi. Zaidi ya vitabu 175
vilinunuliwa baada ya uzinduzi huo.
Katibu
Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akitambulisha viongozi
mbalimbali walioshiriki hafla hiyo wakiwemo baadhi ya mawaziri, wabunge,
madiwani kutoka Manispaa ya Sumbawanga na viongozi wengine wa chama na
Serikali.
Mama
Tunu Pinda mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Mzengo Kayanza Peter Pinda akizungumza katika hafla hiyo ambapo
alimpongeza sana Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya kwa
kuanzisha mpango wa Sumbawanga Ng’ara pamoja na kuandikia kitabu.
Alisema viongozi kama hawa wanaofanya mambo kwa vitendo ndio viongozi wa
mfano wanaotakiwa katika taifa letu.
Naibu
Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anaeshugulia Elimu Mhe.
Kassim Majaliwa akizungumza katika hafla hiyo. Kwa upande wake alisema
kama Wizara wanaipongeza Serikali na wananchi wa Mkoa wa Rukwa kwa
kuanzisha mpango huo wa Sumbawanga Ng’ara na kuunga mkono. Alisema
halmashauri zingine zinatakiwa zijifunze kwa kuanzisha mipango
mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya utunzaji wa mazingira. Mhe. Majaliwa
aliahaidi kununua vitabu 10 vya Sumbawanga Ng’ara.
Mhe.
Pindi Chana, Mbunge Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Njombe akizungumza katika
hafla hiyo. Alimsifu mwandishi wa kitabu hicho cha Sumbawanga Ng’ara
ambaye pia ni muasisi wa mpango huo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi
Stella Manyanya na kusema ni mchapakazi wa kuigwa. Mhe. Chana aliahidi
kununua vitabu 30 vya Sumabwanga Ng’ara kwa ajili ya kuhamasisha usafi
Mkoani Njombe.
Mbunge
wa Kilindi CCM Mhe. Beatrace Shelukindo akizungumza katika hafla hiyo
ambaye naye alipewa fursa na Waziri Mkuu aweze kuzungumza ambapo alisema
Mkoa wa Rukwa umepata kiongozi thabiti ambaye angetamani afanye kazi
katika Mkoa wake wa Tanga. Mhe. Selukindo alinunua vitabu 20 kwa ajili
ya madiwani wa Korogwe ili awape wivu wa kufanya kazi katika maeneo yao.
Mama
Anne wa UNDP akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi wa kitabu cha
Sumbawanga Ng’ara ambapo alifurahishwa na kitendo hicho na kusema yeye
pia ni mdau wa mazingira na hivyo akaahidi kununua vitabu 10 kwa ajili
ya kuviweka katika maktaba yake.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Sabas Katepa akielezea kwa kifupi Mpango
wa Sumbwanga Ng’ara ambapo alisema tangu mpango huo uanzishwe na Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya wananchi wengi wameupokea
vizuri na tayari Mji wa Sumbawanga umeshanza kubadilika ukilinganisha na
kipindi cha nyuma.
Wajukuu
wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere wanaosoma nchini Marekani
wakijitambulisha katika hafla hiyo baada ya kupewa fursa na Waziri Mkuu
Mhe. Mizengo Pinda.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akiendelea na hotuba yake.
Waziri
Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akimkadhi Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj
Salum Mohammed Chima kitabu cha Sumbawanga Ng’ara mara baada ya
kukizindua rasmi.
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @ rukwareview.blogspot.com)
Post a Comment