Tarehe 14 Juni 2013, Wizara ya Afya na Ustawi
wa Jamii kupitia Mpango wa Taifa wa Damu Salama inaadhimisha siku ya wachangia
damu duniani. Kidunia maadhimisho haya yatafanyika Paris nchini
Ufaransa.
Kitaifa Maadhimisho haya mwaka huu
yatafanyika Musoma Mkoani Mara katika kiwanja cha Mkendo siku ya Ijumaa tarehe
14,Juni 2013 kuanzia saa 3 asubuhi na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa
Afya na Ustawi wa Jamii Dr Hussein Mwinyi (MB)
Madhumuni ya maadhimisho haya ni kuongeza
uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa kuchangia damu kwa hiari mara kwa mara
,kuwatambua, kuwaenzi na kuwashukuru walewote ambao wamekuwa
wakichangia damu kwa hiari mara kwa mara bila malipo
yoyote.
Ndugu
Wananchi,
Duniani kote, maelfu ya watu huokolewa maisha
na damu ya watu ambao hawajawahi kukutana nao, watu ambao huchangia damu yao ili
kuwasaidia wengine. Lakini mamilioni bado hawawezi kupata huduma ya damu salama
pindi wanapohitaji. Siku ya leo inatoa fursa ya kipekee kuwashukuru wale watu
maalumu ambao huchangia damu ili kuokoa maisha ya wahitaji. Tunaweza pia
kuongeza uelewa juu ya umuhimu wa kuchangia damu kwa hiari ili Watanzania
wajenge utamaduni wa kuchangia damu kwa hiari mara kwa
mara
Ndugu Wananchi
Kauli mbiu ya siku ya wachangia damu mwaka
huu ni UCHANGIAJI DAMU NI ZAWADI YA MAISHA. Maadhimisho haya yanaenda sambamba
na madhimisho ya miaka 10 ya siku ya wachangia damu
duniani.
Zawadi kubwa ya thamani ambayo sisi binadamu
tunaweza kupeana ni kuchangiana damu, zawadi ambayo inaweza kuokoa maisha na
kutoa nguvu mpya ya maisha kwa watu wengi wanaohitaji tiba
hii.
Kila mmoja wetu anaweza kutoa zawadi ya
maisha kwa kuchangia damu, ndiyo maana dunia inaadhimisha siku hii ili
kuwatambua watu ambao wamekuwa wakitoa zawadi ya maisha kwa kuchangia damu kwa
ajili ya kuokoa maisha ya watu wengine
Ndugu
Wananchi,
Kwanini uchangiaji damu ni zawadi ya
maisha?
Damu ni uhai na ina thamani kubwa, damu
haipatikani viwandani wala kuzalishwa sehemu yeyote ila kwa kuchangiwa na
binadamu wenzetu.
Hivyo zoezi la kuchangia damu ni endelevu na
la kudumu, chupa moja ya damu inaweza kuokoa maisha ya watu zaidi ya mmoja kama
ikigawanywa kwenye mazao ya damu kama vileplasma, chembe sahani na chembe
nyekundu. Damu inaweza kuhifadhiwa kwa muda wa siku 35 kabla ya muda wake wa
kutumika kwisha kulingana na virutubisho vilivyopo. Kutokana na uhifadhi wa damu
kwa muda mfupi ndiyo maana tunasisitiza umuhimu wa watu kuchangia mara kwa mara.
Kitaalamu mwanamume anaweza kuchangia mara nne kwa mwaka na mwanamke mara tatu
kwa mwaka.
Ndugu
Wananchi,
Upatikanaji wa damu kwa wakati huongeza
nafasi ya kuishi kwa wahitaji wa damu, huduma ya damu huokoa maisha ya mamilioni
ya wagonjwa kila mwaka duniani, Yafuatayo ni makundi makuu ya watu ambao huitaji
damu:
•Watoto wadogo hasa walio chini ya umri wa
miaka mitano kutokana na upungufu wa damu unaosababishwa na malaria kali na
magonjwa mengine (50%)
•Wajawazito na wanawake wenye matatizo ya
uzazi (30%)
•Majeruhi wa ajali mbalimbali hasa ajali za
barabarani na watu wanaofanyiwa tiba ya upasuaji
(15%)
•Wale wote wenye magonjwa mbalimbali
yanayosababisha upungufu wa damu kamawagonjwa wa saratani, watu wanaosumbuliwa
na seli mundu na hemophilia (5%)
Ndugu
Wananchi,
Tangu kuanzishwa kwa Mpango wa Damu Salama
Tanzania kumekuwepo na ongezeko la wachangia damu wa hiari kutoka kiasi cha
chupa 5,000 mwaka 2005 hadi kiasi cha chupa 120,000 mwaka 2012. Hata hivyo kiasi
hiki hakikidhi mahitaji halisi nchini ambapo wastani wa chupa 400,000-450,000
zinahitajika kwa mwaka. Hii inaonyesha nakisi kubwa iliyoko ya upatikanaji damu
kwenye hospitali zetu. Nakisi hii mara nyingi imekuwa inafidiwa na ndugu
kuchangia damu ili kuokoa maisha ya mgonjwa. Lengo la Mpango ni kukusanya damu
kwa 100% toka kwa wachangiaji damu wa hiari.
Hata hivyo, katika nchi nyingi Tanzania
ikwemo, hakuna ugavi wa damu salama unaotosheleza, na huduma za damu hukabiliwa
na changamoto ya kupatikana kwa damu ya kutosha, na wakati huo huo kuhakikisha
ubora na usalama wa damu hiyo
Usambazaji wa damu ya kutosha unaweza kuwa wa
uhakika kupitia uchangiaji damu wa mara kwa mara na wa hiari usiohitaji malipo.
Lengo la Shirika la Afya Duniani (WHO) ni kwa nchi zote kupata mahitaji yao yote
ya damu inayohitajika kutoka kwa wachangiaji wa hiari wasiolipwa ifikapo mwaka
2020. Leo hii, ni nchi 62 tu, ambazo usambazaji wa damu kitaifa unatokana na
uchangiaji wa hiari usio na malipo takribani kwa asilimia 100, huku kukiwa na
nchi 40 ambazo bado zinategemea wachangiaji wa familia Tanzania
ikiwemo.
Ndugu
wananchi;
Katika hatua ya kuboresha kazi za ukusanyaji,
upimaji na usambazaji wa damu hospitalini, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
kupitia Mpango wa Taifa wa Damu Salama umeanzisha mfumo wa kisasa wa tekinolojia
ya habari na Mawasiliano-ICT (Blood Establishment computer System) ambapo mpaka
sasa mfumo huu umeshafungwa katika kanda tano ambazo niKanda ya
Ziwa(Mwanza),Kanda ya Kaskazini(Moshi), Kanda ya Nyanda za Juu Kusini(Mbeya),
Kanda ya Mashariki (Dar-es-salaam) na Zanzibar
Katika mfumo huu taarifa muhimu kuanzia kwa
mchangiaji hadi damu inapomfikia mgonjwa zitapatikana kwa urahisi. Vilevile
mfumo huu utasaidia kutambua wachangiaji wa mara kwa mara na hivyo kuweza
kuongeza idadi ya wachangiaji wa kudumu wa mara kwa mara(regular blood donors).
Aidha mfumo huu unasaidia kutambua viashiria mbalimbali ikiwemo kiasi cha
maambukizi ya magonjwa mbalimbali yanayosababishwa kwa kuongezewa damu na hivyo
kuhakikisha usalama wa mgonwa anayepewa damu. Pia mfumo umerahisisha upatikanaji
wa takwimu mbalimbali ikiwemo usambazaji wa damu salama kwenye hosipitali
zetu.
Pia katika hatua za kuhakikisha Mpango unatoa
huduma bora zinazoendana na viwango vya kimataifa, Mpango umeanza mchakato wa
kupata kibali (accreditation) kwa ajili ya kanda za Mpango wa Damu Salama.
Mchakato huu umeanza kwa hatua ya kupitia miongozo na sera katika mtiririko
mzima wa upatikanaji wa damu salama na ukaguzi wa ndani. Katika hatua ya mwanzo
inakadiriwa ifikapo mwaka 2014 vituo viwili vya Damu Salama vitakuwa vimepata
Cheti kutambulisha kuwa vinatoa huduma kulingana na viwango vya
kimataifa
Ndugu
Wananchi,
Mpango umeanzisha matumizi ya mitandao ya
kijamii, hizi ni tovuti zilizoundwa ili kuwezesha na kuongeza ufanisi wa
mawasiliano baina ya mpango na wadau wake. Lengo likiwa kuwafikia zaidi wananchi
wote wa Tanzania waliopo katika mitandao hii. Tovuti hizi ni kama “Facebook,
Tweeter na YouTube”. Uanzishaji wa mitandao hiiinaiwezesha Damu salama
kujulikana, kukuza na kuimarisha mahusiano mazuri kati ya damu salama na
wachangia damu, wafadhili na wadau wengine kupitia kubadilishana habari kwa njia
ya haraka na kwa wakati. Mpango unawasihi na kuwaomba wananchi kujiunga
kufuatilia na kutumia vyombo hivi ili kuongeza ufanisi waMpango wa Taifa wa Damu
Salama na hivyo kuongeza makusanyo ya damu toka kwa wachangiaji wa
hiari.
Ndugu
Wananchi,
Nchini Tanzania mahitaji ya damu yanazidi
upatikanaji. Mpango wa Taifa wa Damu Salama unakabiliwa na changamoto ya
kuhakikishaupatikanaji wa damu salama na ya kutosha ili kuweza kuwasaidia
wagonjwa wanaohitaji damu hospitalini. Mahitaji ya damu kitaifa ni wastani wa
chupa 400,000-450,000. Mpango wa Taifa wa Damu Salama kwa sasa unakusanya
wastani wa chupa 120,000 kwa mwaka(26%). Hii inaonyesha nakisi kubwa iliyoko ya
upatikanaji damu kwenye hospitali zetu. Nakisi hii mara nyingi imekuwa inafidiwa
na ndugu kuchangia damu ili kuokoa maisha ya mgonjwa. Lengo la Mpango ni
kukusanya damu kwa 100% toka kwa wachangiaji damu wa hiari.Mikakati kadhaa
imewekwa kukabiliana na changamoto hii kama tutakavyoona
baadaye.
Changamoto nyingine ni kama
ifuatavyo;
Uelewa mdogo katika jamii kuhusu suala zima
la uchangiaji damu kwa hiari kwani mfumo uliozoeleka ni ndugu wa mgonjwa
kuchangia damu
Uhamasishaji usiotosheleza toka kwa viongozi
mbalimbali wa jamii,wanasiasa,viongozi wa dini
nk.
Uuzwaji wa damu usio halali hospitalini jambo
mbalo linawakatisha tamaa wachangia damu wa hiari
Matumizi yasiyo sahihi ya damu katika
hospitali na
Miudombinu hafifu hususan barabara duni
wakati wa kukusanya na kusambaza damu
Ndugu Wananchi
Mpango wa Taifa wa Damu Salama umeweka
mikakati ili kukabiliana na changamoto na kufikia malengo kama
ifuatavyo;
Kufanya kampeni ya kuhamasisha uchangiaji
damu katika jamii (Community Campaign), Kampeni hii ina lengo la kuhakikisha
upatikanaji wa damu ya kutosha wakati wanafunzi ambao ndio wadau wakubwa wapo
likizo
Kuongeza vituo vidogo vya kuchangia damu-
“Blood collection satellite sites” katika sehemu mbalimbali za nchi. Kwa sasa
Mpango una vituo vidogo vinne Dar-es-salaam- Mnazi Mmoja , Dodoma, Lindi na
Morogoro ambavyo vina uwezo wa kukusanya chupa za damu 18,000 kwa
mwaka
Kushirikiana na uongozi wa mkoa kupitia
mganga mkuu wa mkoa ili wilaya zitenge bajeti ya kukusanya damu kwa kushirikiana
na Mpango wa Taifa wa damu salamaKufanya mkakati wa kujua matumizi halisi ya
damu (Blood need assessment) nchini na kuendelea kuhamasisha madaktari, wauguzi
na watumishi wa maabara juu ya matumizi sahihi ya
damu
Kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali
Puplic Private Partnership(PPP) kuhakikisha Mpango unafikia malengo ya kukusanya
chupa za kutosha za damu
Kuendelea kuelimisha jamii kuhusu damu
haiuzwi kwa kutumia vyombo vya habari na vipeperushi pia kutumia vifungashio vya
damu (Blood bag) vyenye ujumbe “DAMU HAIUZWI”
Kuendelea kuelimisha na kuhamasisha jamii
(nje ya shule na vyuo) umuhimu wa kuchangia damu kwa
hiari
Kutoa majibu, na ushauri nasaha ndani yawiki
mbili mpaka nne baada ya mtu kuchangia damu lengo ni kufikia 75% ya wachangiaji
damu wa hiari ifikapo mwishoni mwa 2014. Kwa sasa Mpango umeweza kutoa majibu na
ushauri nasaha kwa 58% ya wachangiaji damu wa
hiari.
Kuanzisha utaratibu wa kutuma ujumbe mfupi wa
maandishi kwa njia ya simu kwa wachangia damu. Ujumbe huo utakuwa wa
kuhamasisha, kumkumbusha mchangiaji siku ya kuchangia tena damu
n.k
Kuongeza utengenezaji wa mazao mbalimbali ya
damu (Blood Products) toka30% ya sasa mpaka 50% mwaka
2014.
Kuongeza kiwango cha asilimia ya wachangia
damu wa mara kwa mara kutoka 20% kwa sasa (Repeat donors), hadi 50%ifikapo mwaka
2015 . Mpango utahakikisha unatembelea taasisi kwa ajili ya kuchangia damu
angalau mara mbili kwa mwaka.
Ndugu
Wananchi;
Uchangiaji damu wa hiari wa bila malipo
yoyote na wa mara kwa mara ni msingi wa upatikanaji wa damu salama na ya
kutosha. Wachangiaji damu wa kujirudia ni salama kwani damu yao hainakiwango
kikubwa cha maambukizo ya magonjwa yanayoweza kuenezwa kwa njia ya damu. Lengo
la Shirika la Afya Duniani (WHO) ni kwa nchi zote kupata mahitaji yao yote ya
damu inayohitajika kutoka kwa wachangiaji wa hiari wasiolipwa ifikapo mwaka
2020
Ndugu
Wananchi;
Natoa rai/ujumbe kwa Watanzania kujenga
utamaduni wa kuchangia damu kwa hiari mara kwa mara ili nchi iwe na akiba ya
damu ya kutosha , kwani asilimia moja ya Watanzania wakiamua kuwa wachangiaji
damu wa kujirudiaMpango wa Taifa wa Damu Salama utaweza kukidhi mahitaji ya damu
nchini.
NAMALIZIA KWA KUSEMA NAOMBA WANANCHI
WAJITOKEZE KWA WINGI SIKU HIYO ILI TUONYESHE MSHIKAMANO NA KUTOA ZAWADI YA
MAISHA KWA KUCHANGIA DAMU. PAMOJA INAWEZEKANA


Post a Comment