MADAKTARI
wa hospitali ya St. Joseph iliyoko Central New York walikuwa katika mchakato wa
kuanza upasuaji wa kunyofoa viungo katika mwili wa mwanamke aliyekufa ndipo
mwanamke huyo akafumbua macho yake. Alikuwa angali hai.
Kosa hilo kubwa mno limeigharimu hospitali hiyo Dola za Marekani 6,000 baada ya
uchunguzi wa pamoja na ongezeko la faini ya Dola za Marekani 16,000 baada ya
mgonjwa mwingine kuanguka na kuumia kichwani wakati alipotelekezwa bila
kuhudumiwa mwaka 2011, kwa mujibu wa ripoti za gazeti la Syracuse
Post-Standard.
Colleen S. Burns wa North Syracuse, mjini New York, mwenye umri wa miaka 41,
alikuwa amelazwa hospitalini hapo Oktoba 2009 kwa tatizo la kujizidishia dozi
ya dawa.
Sababu ya mfululizo wa makosa katika tathimini, madaktari waliamini kwamba
mwanamke huyo alikuwa amekufa na kuanza mchakato wa kuchangisha viungo.
Uchunguzi wa Idara ya Taifa ya Afya kuhusu tukio hilo uligundua kwamba pale
Burns alipolazwa kwanza, waliruka matibabu yaliyopendekezwa kwamba ingeweza
kuzuia dawa hizo alizotumia - Xanax, Benadryl na zile za kulainisha misuli -
zisifyonzwe na tumbo lake na matumbo.
Pia hawakufanya vipimo vya kutosha kuona kama hakuwa na dawa zilizobaki au
kufanya kaguzi za kutosha kwenye ubongo.
Sababu hawakufanya kaguzi hizi za kutosha, madaktari waliamini kwamba ubongo wa
Burns haukuwa ukifanya kazi, wakati uhalisia kujizidishia huko dozi kulimfanya
azimie kwa muda mrefu.
Baada ya madaktari kusema ubongo wake ulikuwa haifanyi kazi, familia yake
ilikubali kumwondoa kwenye mashine za kusaidia kupumua na viungo vyake kutolewa
kwa ajili ya kuchangia wenye mahitaji.
Lakini siku hiyo kabla viungo hivyo havijaondolewa, muuguzi mmoja alifanya
tendohiari na kugundua kwamba Burns alikuwa bado ana fahamu.
Alikunja vidole vyake chini ya moja ya miguu ya Burns na vidole vyake vya
mguuni vikajikunja kwenda chini, ishara kwamba alikuwa angali hai.
Na hiyo haikuwa ishara pekee ya uhai. Wakati alipokuwa akipelekwa kwenye chumba
cha upasuaji, matundu ya pua ya Burns yalikuwa yakicheza na kuonesha kwamba
alikuwa akipumua mwenyewe kutoka kwenye kipumulio.
Pia midomo yake na ulimi navyo vilikuwa vikitikisika.
Lakini madaktari walipuuza ugunduzi wa muuguzi huyo ambao uliashiria kwamba
Burns bado yuko hai, na wakaendelea na upasuaji bila kujali.
Kabla ya mchakato huo, Burns alikuwa amechomwa sindano ya kutuliza ya Ativan,
lakini si kitulizo hicho au ugunduzi wa uhai uliorekodiwa kwenye karatasi ya
daktari kwa ajili ya mchakato huo.
Haikuwa hivyo hadi Burns alipofumbua macho yake kwenye chumba cha upasuaji
ndipo mchakato huo ulipositishwa.
Si Burns au familia yake iliyoishitaki hospitali hiyo kwa kuzembea kazi.
Miezi 16 baadaye, Burns akafanikiwa kujiua.
Mama yake, Lucille Kuss alisema binti yake hakuwa amefadhaishwa na tukio hilo.
"Alikuwa amehuzunishwa mno kwamba haikuwa imebadilisha chochote
kwake," alisema Kuss.
Hospitali hiyo hata haikuripoti tukio hilo, wala kufanya uchunguzi wao binafsi.
Iliendelea hivyo hadi baada ya Post-Standard kuanza uchunguzi wao ambao
hospitali hiyo hakutoa maelezo ya aina yoyote kwa kile kilichotokea.
on Tuesday, July 16, 2013
Post a Comment