Na Prince Akbar, - BIN ZUBEIRY
AZAM
FC imeendeleza wimbi lake la ushindi katika mechi zake za kujitayarisha
na msimu, baada ya jioni ya leo kuitandika Ashanti United ya Ilala
iliyorejea Ligi Kuu mabao 5-1 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi,
nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Huo unakuwa ushindi wa pili mfululizo, baada ya wiki iliyopita kuichapa kombaini ya timu ya majeshi la Kujenga Taifa (JKT), 1-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, bao pekee la beki Luckson Kakolaki.
Huo unakuwa ushindi wa pili mfululizo, baada ya wiki iliyopita kuichapa kombaini ya timu ya majeshi la Kujenga Taifa (JKT), 1-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, bao pekee la beki Luckson Kakolaki.
Katika mchezo wa leo, mabao ya Azam yalifungwa na Seif Abdallah Karihe mawili dakika za 38 na 52, Kipre Herman Tchetche kwa penalti dakika ya 23, Jabir Aziz Stima dakika ya 70 na Brian Umony dakika ya 78.
Bao pekee la Ashanti lilifungwa na mshambuliaji mkongwe, Said Maulid ‘SMG’ dakika ya 82 baada ya kuwazidi kasi na maarifa wachezaji wa Azam.
SMG aliyeingia kipindi cha pili, alionyesha uwezo mkubwa na kuwakumbushia mashabiki enzi zake anang’ara na klabu ya Yanga ya Dar es Salaam.
SMG alikuwa anacheza Angola tangu mwaka 2007 na sasa amerejea nyumbani na kuamua kujiunga na Ashanti kumalizia soka yake.
Alikwenda Angola akitokea Yanga SC aliyoichezea tangu mwaka 2001 akitokea Simba SC iliyomsajili kutoka Kigoma mwaka 2000.
SMG alitamani kuanza kucheza tena Tanzania tangu Januari mwaka huu na aliomba nafasi katika klabu yake ya zamani, Yanga SC wakamkatalia wakidai amezeeka, lakini kwa soka aliyoonyesha leo na kama ataendelea hivyo katika Ligi Kuu, wana Jangwani watajilaumu.
Post a Comment