Na Emmanuel
Richard Makundi
Rais wa mpito wa Misri ameliapisha baraza lake
jipya la mawaziri huku akiwapa nafasi viongozi wenye msimamo wa kati na pia
akiwajumuisha wanawake wawili kwenye Serikali mpya.
Baraza jipya la
Misri likiwa kwenye picha ya pamoja
Reuters
Serikali mpya inaongozwa na waziri mkuu, Hazem
el-Beblawi ambaye kwa taaluma ni mchumi, Abdel-Fattah al-Asisi ambaye ataendelea
kushikilia nafasi yake ya waziri wa ulinzi na pia Kama naibu waziri mkuu wa
kwanza.
Waziri wa masuala ya ndani ambaye aliteuliwa na
rais aliyepinduliwa, Mohamed Ibrahim ataendelea kushikilia wadhifa wake, huku
Nabil Fahmy ambaye aliwahi kuwa balozi wa Misri nchin Marekani, sasa atakuwa
Kama waziri wa mambo ya nje.
Akisisitiza kwanini baraza lake limejumuisha
viongozi wenye msimamo wa Kati, rais wa mpito, Adly Mansour amesema amazingatia
mahitaji ya nchi huku akitangaza nafasi tatu za wanawake kwenye baraza
lake.
Wizara walizopewa wanawake hao ni pamoja na
wizara ya habari, wizara ya afya na wizara ya mazingira, uteuzi ambao unaonekana
haukutarajiwa na wananchi wengi.
Baraza Hilo jipya lina jumla ya mawaziri
thelathini na wanne huku waziri mkuu el-Beblawi akiwajumuisha hajajumuishwa
kwakuwa ni waziri mkuu tayari.
Hata hivyo baraza hili jipya lililotangazwa na
rais Mansour limeonekena kawa la tofauti kutokana na viongozi wengi
waliotangulia kujumjisha wanawake wasiozidi wawili kwenye mabaraza Yao.
Hata hivyo uteuzi wa mawaziri hao haujajumuisha
kiongozi yeyote wa juu toka vyama vya kiislamu huku msemaji wa rais akisema
nafasi nyingine wamewekewa viongozi wa chama cha Muslim Brotherhood.
Punde Mara baada ya kutangazwa kwa baraza na
kuapishwa, viongozi wa chama cha Muslim Brotherhood wamesema hawatashiriki
kwenye Serikali ambayo imeingia madarakani kwa kutumia nguvu za kijeshi na kuapa
kufanya maandamano zaidi.
Wafuasi wa Muslim Brotherhood wanalikosoa jeshi
la nchi hiyo kwa kuipindua Serikali halali na kuharibu demokrasia ya
Misri.
Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema kawa
baraza hilo sio jipya sana kwakuwa karibu mawaziri saba waliokuwa kwenye
Serikali iliyoangushwa wameendelea kushikilia nyadhifa zao.
Msemaji wa chama cha Muslim Brotherhood, Gehad
El-Haddad amelikashifu baraza hilo akisema ni batili na halina mamlaka ya
utawala kwakuwa hata Serikali yenyewe haijachaguliwa kidemokrasia.
Chanzo: kiswahili.rfi
Post a Comment