Na
Mwandishi Maalum
Baraza Kuu la Usalama la
Umoja wa Mataifa, jana jumatano liliendesha majadiliano ya wazi kuhusu usalama
wa waandishi wa habari katika maeneo yenye migogoro.
Majadiliano hayo
yaliratibiwa na Marekani ambaye ni Rais wa Baraza hilo kwa mwezi huu wa Julai,
na kuhudhuriwa na waandishi wanne wa kimataifa ambao walipata fursa ya
kuelezea masahibu wanayokumbana nayo wakati wa kitekeleza majukumu
yao.
Majadiliano kuhusu suala
la usalama wa waandishi wa habari katika maeneo yenye migogoro ni ya kwanza
kufanyika ndani ya Baraza hilo, tangu lilipopitisha Azimio namba 17 38 mwaka
2006 lililokuwa likizungumzia suala hilo. Aidha hii pia ni mara ya kwanza kwa
waandishi wa kimataifa kuzungumza ndani ya Baraza Kuu la
Usalama.
“
Hapa nilipo mimi ni maiti anayetembea , ninatembea pasi kujua nani anaweza
kuondoa uhai wangu,wakati wowote naweza kupotea maisha. naweza kuuawa hata na
kijana mdogo ilimradi ana silaha”
Kauli hiyo ilikuwa ni ya Bw. Mustafa Haji Abdinur anayeandikisha AFP
akitoka Somalia. Na kuongeza kwamba rafiki zake wengi ambao ni waandishi
wenziye tayari wameshapotea maisha na kwamba kwa yeyé kuwa hai mpaka sasa ni
kama bahati lakini ni suala la wakati tu.
Naye Bi. Cathleen Carrol
ambaye ni Mhariri Mtendaji wa Associated Press na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya
Kamati ya Kuwalinda Waandishi ( CPJ) pamoja na kuelezea kwa uchungu mkubwa
matukio ya mauaji yaliyowakumbua waandishi wenzake katika maeneo mbalimbali
duniani anasema, katika shirika lao kuna eneo ambalo limetengwa maalum
kwaajili ya kuwaenzi waandishi wote ambao wamepoteza maisha katika utekelezaji
wa majukumu yao.
Kwa
upande wake, mwandishi Richard Engel wa NBC news, yeyé pamoja na kuelezea
mikasa mbalimbali ambayo amekwisha kumbana nayo yakiwamo ya kutekwa wakati
akiripoti matukio ya migogoro, yeyé alikwenda mbalia zaidi kwa kuuliza ni nani
hasa mwandishi wa habari.
Bw,
Engel alieza kwamba ulinzi wa waandishi wa habari hivi sasa unakuwa mgumu sana
tofauti na miaka ya nyuma kutokana na kile alichosema kuibuka kwa makundi mengi
yanayofanya kazi za waadishi wa habari.
“
Wakati tukijadili hoja hii ya usalama wa waandishi wa habari, pengine pia ni
muhimu tukajiuliza hivi ni nani hasa mwandishi wa habari, je mwanaharakati
anaye shika video au kamera na kalamu je naye ni mwandishi, au je na yule
mwanamgambo mwenye silaha lakini naye ameshika kamera na kupiga picha je
naye ni mwandishi” akahoji Bw, Engel
Anasema kwamba ni jambo la
kawaida hivi unapokwenda kwenye tukio fulani kukutana na makundi ya watu kila
mmoja akiwa ameshika kamera yake akichukua matukio, na katika mazingira kama
haya, ni vigumu kwa vyombo vya ulinzi na usalama kutofautisha nani hasa ni
mwadishi aliyesomea na kubobea kwenye fani hiyo na yupi mwanarakati.
Kwa
maoni yake anasema pamoja na hamu ya kila mtu kutaka kutaka kukukusanya habari
na kuzisambaza kupitia mitandao ya kijamii, ni vime kujiuliza nani anastahili
na anapwashwa kupewa ulinzi anapotimiza majukumu yake na kwa vyovyote vile
anasema kama ilivyo kwa wanadiplomasia ambao wanakinga vilevile waandishi
waliosomea na wenye weledi na taaluma yao wanatakiwa kupewa
ulinzi.
Majadiliano hayo
yalifunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Eliasson, na
yalikuwa na mvuto wa ina yake hasa kutoka na kauli zilizokuwa zikitolewa na
baadhi ya wachangiaji.
Kwa
upande wake Naibu Katibu Mkuu alieleza kwamba hujuma dhidi ya waandishi wa
habari ni jambo lisilokubalika kwa kile alichosema ni kubinya uhuru wa
upatikanaji na utoaji wa habari, lakini pia ni ukiukwaji wa uhuru wa kujieleza.
Akalipongeza Baraza kwa kuitisha mjadala
huo
Akasema karne iliyopita
waandishi wa habari wapatao 600 walipoteza maisha katika matukio mbalimbali na
wengine wakiishia magerezani, huku asilimia 90 ya matukio hayo hakuna hatua
zozote za kisheria zilizochukuliwa.
Pamoja na wachangiaji wengi
kukiri kwamba mazingira ya ufanyaji kazi kwa waandishi wa habari yamezidi
kuwa magumu na hatari, walielezea pia kwamba mazingira hatarishi hayapo tu
katika maeneo yenye vita bali hata katika nchi wazofanyia kazi. Ambapo takwimu
kutoka CPJ zinaonyesha katika kila waandishi watano kati ya sita wanauliwa
wakiwa ndani ya nchi zao.
Wengi wa wazungumzaji
walieleza kwamba baadhi ya waandishi ama wamekuwa wakitishiwa maisha yao na
familia zao au hata kupoteza maisha kwa kuandika na kuchapicha habari
zinazofichua vitendo vya rushwa , vitendo vya jinai au kashfa zinazohusu
makundi mbalimbali ya jamii na vilevile kuandika habari za uchochezi kati ya
kundi moja na jingine..
Wengine wakaenda mbali kwa
kusema wakati mwingine waandishi wenyewe wanajiweka katika mazingira ya hatari
kwa kukiuka misingi ya kazi zao, kwa kuandika habari zinazopendelea upande
mmoja, au kufanya kazi kinyume cha matakwa na matarajio ya yule anayemfanyia
kazi.
Wazungumzaji hao wakatoa
wito kwa Baraza kuu la Usalama kuangalia namna bora ya kuboresha ulinzi wa
waandishi wa habari katika mazingira hatarishi kama vile vita na migogoro na
pia wakatoa wito wito kwa waandishi wa habari kuzingatia misingi ya taaluma
zao na kuepuka kujingiza katika mitengo isiyo ya
lazima.
Suala lingine
lililozungumwa kwa kina ni lile la kutofikishwa mbele ya mkono wa sheria watu
wanaotuhumiwa kuwahujumu waandishi wa habari.
Post a Comment