Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

BREAKING NEWS: RAIS WA MISRI MOHAMED MORSI AMEPINDULIWA NA JESHI USIKU HUU


Generali Abdul Fattah al-Sisi akizungumza moja kwa moja kutoka televisheni ya taifa ya Misri

===============

Hatimaye jeshi la Misri limejitokeza live kwenye televisheni ya Misri na kutangaza rasmi kuifuta katiba ya nchi hiyo muda mfupi kutoka sasa

Generali Abdul Fattah Al-Sisi, amesema kuanzia sasa mwanasheria mkuu wa mahakama ya katiba ndiye atakuwa anakaimu madaraka yote ya raisi na kutangaza rasmi kutomtambua bwana Mohamed Morsi

Wapinzani wa raisi Morsi waliandamana na kukusanyika katika uwanja wa Tahrir Square na kuonekana wakishangilia kwa nguvu wakati Generali Abdul akitoa tangazo hilo la kumpindua raisi Morsi

Mchakato huo wa kumng'oa bwana Morsi ni kufuatia maandamano ya umma ya siku nne kumtaka raisi huyo aachie madaraka na kutii amri ya jeshi ambayo imeisha usiku wa leo jumatano saa nne usiku kwa saa za Tanzania

Aidha kituo cha TV kilichokuwa kikimilikiwa na bwana Morsi cha Muslim Brotherhood kilizimika sekunde chache baada ya Generali Abduli kumaliza hotuba ya kumpindua rais MORSI aliyeingia madarakani baada ya kumpindua aliyekuwa raisi wa nchi hiyo .
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top