
Na Elizabeth Ntambala
Sumbawanga
Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinadaiwa kumvua uanachama wake
Diwani wa kata ya Izia katika Manispaa ya Sumbawanga, Field Kasitu kwa
tuhuma ya kukisaliti chama hicho.
Taarifa zilizopatikana
kutoka ndani ya chama hicho zinaeleza kuwa Kasitu amefukuzwa baada
yakuonekana akitambulishwa bungeni mjini Dodoma akiwa mmoja kati ya
viongozi waliotoka mkoani Rukwa na kumsindikiza Mbunge wa Sumbawanga
Mjini Aeshi Hilary baada ya kurejeshewa ubunge wake na Mahakama ya Rufaa
kufuatiwa kutenguliwana Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga mwaka mmoja
uliopita.
Tukio hilo lilionekana kuwakera baadhi ya viongozi
na wanachama wa CHADEMA ambao walihoji kuwa iweje Diwani huyu ajiunge na
CCM katikakushangilia kushinda kesi na kurejeshewa nafasi yake Mbunge
huyo ihali wao CHADEMA kupitia aliyekuwa mgombea wao Nobert Yamsebo
kupinga ushindi wake.
Pamoja na
tuhuma hizoKasitu alisema kuwa wanaomlaumu juu ya hilo ni wachanga wa
kisiasa na hawajui mtazamo wake katika maisha yake ya kisiasa.
Kauli
hizo za Kasitu zilionekana kuzidi kuwakera viongozi wake wa wilaya
ambapo walimwandikia barua ya kumtaka kujieleza kwanini asichukuliwe
hatua za kinidhamu kwa kosa la kudaiwa kufanya usaliti.
Hatua hiyo ilielezwa kushikiwa bango na Katibu wa chamahicho ngazi ya wilaya Omeli Nkulu ambaye alimwandikia barua.
Mmoja
ya wajumbe wa Kamati Tendaji ya wilaya ambaye hakutaka jina lake
litajwe alisema kuwa licha ya kutakiwa kujieleza tayari Diwani huyo
ameandikiwa barua ya kuvuliwa uanachama japokuwa wapo baadhi ya wajumbe
wa kamati hiyo ambao wanaopinga hatua hiyo.
Katibu CHADEMA
mkoa Ozemu Chapita alipoulizwa juu ya sakata hilo alisema kuwa anafahamu
kuwa Kasitu alipewa barua ya kujieleza ndani ya siku 14,lakini haungi
mkono hatua ya kuvuliwa uanachama.
"Mimi binafsi siungi mkono
hatua ya kumvua uanachama kwani itatufanya tugawanyike katika kipindi
hiki, jambo nisingependa lilotekee kwetu."alisema Chapita.
Kasitu
ni Diwani aliyepata nafasi hiyo akitokea CCM ambapo alijiunga na
CHADEMA baada ya kile kinachodaiwa kufanyiwa mizengwe wakati wa mchakato
wa kura za maoni na kukosa nafasi ya kugombea kupitia chama hicho,
hivyo kuamua kujiunga na CHADEMA na kumbwaga mpinzani wake kutokea CCM
Timoth Makaza.
Mwisho.


Post a Comment