Ubalozi
wa Tanzania nchini Marekani umemfanyia hafla fupi ya kumtambulisha Mhe.
Balozi Liberata Mulamula kwa kwa Whe. Mabalozi wa nchi jirani na nchi
marafiki wa Tanzania wakiwemo viongozi wa jumuiya mbalimbali za
Watanzania DMV. Kwenye picha Kaimu Balozi na Mkuu wa Utawala na Fedha
Mama Lily Munanka (kati) akimkaribisha Mhe. Balozi Liberata Mulamula
mara tu alipowasili Ubalozini hapo akiambatana na familia yake, kulia ni
Charles Gray ambaye ni Balozi wa hiari anayeitangaza Tanzania nchini
Marekani na anayeishi Pennsylvania kwenye mji uitwao Bala Cynwyd.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Charles Gray.
Mhe. Liberata Mulamula akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowassa.
Kaimu
Balozi na Mkuu wa Utawala na Fedha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani,
Mama Lily Munanka akiongea machache yakiwemo kuwakaribisha Whe.
Mabalozi na Viongozi mbalimbali wa Jumuiya za Watanzania DMV kwenye
Hafla hiyo fupi na baadae kumkaribisha Mhe. Balozi Liberata Mulamula
kuongea nao.
Mhe.
Balozi Liberata Mulamula akiongea machache yakiwemo kuwashukuru Maafisa
na wafanyakazi wa Ubalozi kwa kuandaa Hafla hiyo fupi ya kumtambulisha
kwa Whe. Mabalozi wa nchi jirani na nchi marafiki wa Tanzania na
Viongozi mbalimbali wa Jumuiya za Watanzania DMV wakiwemo wanahabari wa
DMV pia alielezea kwamba leo Alhamisi July 18, 2013 alipeleka hati yake
ya utambulisho kwa Rais Barack Obama na anafuraha kukutana nao hapo
Ubalozini na hii isiwe mwisho wanakaribishwa muda wote wajisikie wapo
nyumbani.
Mhe.
Balozi Liberata Mulamula akimkaribisha Afisa Mindi Kasiga ili aongoze
kuimba wimbo wa Tanzania, Tanzania, nakupenda kwa moyo wote. Mindi
Kasiga ndiye aliyekua mshereheshaji wa Hafla hiyo.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akitambulisha familia yake kutoka kushoto ni mwanaeTanya, Alvin na Mumewe Bwn. George Mulamula.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akifanya tosi.
Whe. Mabalozi, Viongozi mbalimbali wa Jumuiya za Watanzania DMV, wageni waalikwa wakitosi pamoja na Mhe. Balozi.
Post a Comment