MKURUGENZI WA Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Nape Nnauye
amesema suala la uchaguzi wa Meya wa Mji wa Arusha limefikia tamati na
kamwe uchaguzi huo hautafanyika tena. Nnauye alisema hayo alipozungumza
na MTANZANIA jana, huku akiwataka wananchi wa Jiji la Arusha kupuuza
kauli za vitisho zinazotishia kumwondoa madarakani Meya wa Jiji,
Gaudence Lyimo.
Kauli ya Nnauye inafuatia kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa Madiwani wa Chadema Arusha Isaya Doita, aliyesema kuwa ushindi wa udiwani wa chama chao katika kata nne za mji huo ni chachu katika msimamo wa chama chao kutaka uchaguzi wa Meya wa Arusha urudiwe.
Doita akiamini kuwa Lyimo alichaguliwa kwa mizengwe, alisema ana imani muda si mrefu Jiji la Arusha litapata meya ambaye amechaguliwa kwa misingi ya sheria.
Hata hivyo, siku chache baadaye Katibu wa Chadema wa Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa alisema suala la nafasi ya umeya siyo tena ajenda ya chama hicho.
Akizungumzia suala hilo jana, Nnauye alisema CCM imezoea kusikia kauli mbalimbali za vitisho zinazotolewa Chadema na kuwataka wananchi wa Arusha kuzipuuza kauli hizo.
“Ni kazi yao vitisho nia yao ni kutaka watu wasifanye shughuli zao, lakini suala la meya yupo pale na ataendelea kuwapo kwani uchaguzi ulishafanyika na hautafanyika tena.
“Kazi iliyobaki sasa kwa wananchi wa Arusha ni kujenga mji wao kwa kufanya kazi, watu wafanye kazi zao wala hakuna sababu ya kuhofia kauli za vitisho.
“Ni upuuzi kuanza kuzungumzia kila siku suala la Arusha, waliopewa dhamana wawajibike kilichobaki ni kufanya kazi, waache kusikiliza upuuzi,” alisema Nnauye.
MTANZANIA

Post a Comment