Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Saidi Mwema akipokea zawadi ya picha
iliyochorwa picha yake kutoka kwa mwakilishi wa kikundi cha ulinzi
shirikishi cha shehia ya Mkele, Maalim Rashidi wakati wa sherehe za
uzinduzi wa upanuzi wa zahanati ya Polisi, Ziwani Visiwani Zanzibar
jana. Picha zote na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
Nassir
Hassan wa kikundi cha Kung Fu cha Shehia ya Nyerere akifanya onyesho la
kung fu jana Visiwani Zanzibar wakati wa sherehe za uzinduzi wa upanuzi
wa zahanati ya Polisi, Ziwani Visiwani Zanzibar jana. Picha na Hassan
Mndeme-Jeshi la Polisi. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Saidi Mwema akipokea zawadi ya matunda
aina ya shokshok kutoka kwa mwakilishi wa kikundi cha ulinzi shirikishi
cha shehia ya Ubago, Asha Suba wakati wa sherehe za uzinduzi wa
upanuzi wa zahanati ya Polisi, Ziwani Visiwani Zanzibar jana.
Wanafunzi
wa kikundi cha sanaa cha Shule ya Msingi Matopeni Unguja, wakiimba
nyimbo ya kuhimiza vijana kuacha dawa za kulevya, baada ya IGP Saidi
Mwema kufanya uzinduzi wa upanuzi wa zahanati ya Polisi, Ziwani,
Visiwani Zanzibar jana.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Saidi Mwema akipokea zawadi ya mfano wa
mashua kutoka kwa mwakilishi wa kikundi cha ulinzi shirikishi cha shehia
ya Stone Town, Saidi Mkweche wakati wa sherehe za uzinduzi wa upanuzi
wa zahanati ya Polisi, Ziwani Visiwani Zanzibar jana.
Hapsa
Omar wa kikundi cha Kung Fu cha Shehia ya Nyerere akifanya onyesho la
kung fu dhidi ya mpinzani wake Nassir Hassan jana Visiwani Zanzibar
baada ya IGP Saidi Mwema kufanya uzinduzi wa upanuzi wa zahanati ya
Polisi, Ziwani Visiwani Zanzibar jana.
Hapsa Omar(kulia) na Habiba Nassor wa kikundi cha Kung Fu cha Shehia ya Nyerere wakifanya onyesho la kung fu.
Post a Comment