
Mwaka 1956 utawala wa Makaburu uliwakamata watu 156 akiwamo Nelson Mandela. Walifungulia mashtaka ya uhaini. Na baada ya hapo ikapigwa marufuku ya mikutano na mikusanyiko yoyote ya kisiasa. Na Nelson Mandela anasema;“ Marufuku ile ilikuwa haina maana yeyote, maana, karibu wajumbe wote wa Kamati Kuu ya Taifa ya ANC ( Wajumbe wa NEC) walikuwa miongoni mwa waliokamatwa. Hivyo, kila jioni, tukiwa kwenye mapumziko yetu gerezani, tulikusanyika na kuongea mambo yetu ya siasa!”- Nelson Mandela.
Maggid
0754 678 252


Post a Comment