Ghulam Azam, kiongozi wa chama cha kiislamu
cha Jamaat-e-Islami ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka 90 Reuters |
Na Emmanuel
Richard Makundi
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita
nchini Bangladesh imemuhukumu kifungo cha miaka 90 jela kiongizi wa kiislamu
Ghulam Azam baada ya kumkuta na hatia ya makosa yote matano yaliyokuwa
yakimkabili kuhusiana na vita vya harakati za ukombozi mwaka 1971 toka kwa nchi
ya Pakistan.
Ghulam Azam mwenye umri wa miaka 90 hivi sasa
anatuhumiwa kushiriki kuunda vikundi vya uasi wakati wa vita hivyo ambapo
vilihusika kupanga, kutekeleza mauaji na kushiriki vetndo vya ubakaji dhidi ya
raia.
Wafuasi wa chama cha kiislamu cha Jamaat
--Islam kilichokuwa kinaongozwa na Ghulam toka mwaka 1969 hadi 2000
wamekabiliana na polisi nje ya mahakama hiyo kabla na baada ya hukumu
kusomwa.
Mahakama hiyo imemkuta na hatia ya makosa yote
matano ikiwemo uchochezi, kupanga njama kutekeleza mauaji, kushindwa kuzuia
mauaji, ubakaji na uhalifu dhidi ya binadamu.
Ghulam mwenyewe amekanusha kuhusika na
machafuko ya nchini mwake wakati wa harakati za kupigania uhuru wake toka kwa
taifa la Pakistan na kudai kuwa kesi yake ni yakisiasa.
Wafuasi wa Ghulam wameapa kufanya maandamano
kupinga hukumu hiyo ambayo nao wanadai ilichochewa kisiasa.
Awali mwendesha mashtaka wa Serikali aliiomba
mahakama kumuhukumu kunyongwa Ghulam kutokana na makosa ambao aliyatekeleza
wakati akiwa kiongozi wa chama.
Zaidi ya watu laki tatu wanaelezwa kupoteza
maisha nchini Bangladesh wakati wa vita vya uhuru, huku Ghulam akitajwa kuhusika
kwa sehemu kubwa kutekeleza mauaji hayo.
Source - kiswahili.rfi.fr
Post a Comment