Na Anna Nkinda – Maelezo
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amewataka wanawake wa dini zote nchini kutokubaguana kutokana na itikadi zao za vyama vya siasa bali wawe mstari wa mbele kuhubiri amani na upendo.
Mama Kikwete aliyasema hayo jana wakati akiwafutarisha wanawake wa dini mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mama
Kikwete alisema kuwa ukosefu wa amani ukitokea katika nchi wanawake na
watoto ndiyo wahanga wakubwa hivyo basi wasikubali watu kuwadanganya
bali wawe na msimamo na umoja ili waweze kuilinda amani ambayo ndiyo
silaha pekee ya kuwaletea ukombozi iliyoasisiwa na wazee wa nchi yao.
“Ninawashukuru
kwa kuacha shughuli zenu na kuitikia wito wangu wa kuja na kufuturu
pamoja nami, nawatakia mfungo mwema nini nyote mnaofunga ili Mwenyezi
Mungu awakubalie heri zenu nanyi msiofunga Mwenyezi Munguawabariki
katika maisha yenu ya kila siku”, alisema Mama Kikwete.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanawake wa Kiislamu Tanzania
Taifa (BAKWATA) Shamim Khan alimshukuru Mama Kikwete kwa upendo wake wa
kuwaalika wanawake hao kupata futari ya pamoja.
Mama
Khan alisema kuwa kukutana kwao kumewafanya wajifunze kuwa wakitaka
amani ni lazima washirikiane bila ya kujali rangi, dini na kabila kwani
wanawake wote wanamatatizo yanayofanana ambayo wanaweza kuyatatua kwa
pamoja bila ya kuangalia kuwa huyu ni mkristo au muislamu na wakikaa
pamoja amani inapatikana.
Naye Olive
Lwema ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanawake wakristo Tanzania
alisema kuwa aliposikia wamepata mwaliko huo alifurahi sana kwasababu
wanapokutana wanawake ambao ni wazazi wa watoto wa taifa, wake wa waume
wanaoongoza nchi hakuna jambo litakaloharibika na ameshuhudia kwa kuona
nyuso za ushirikiano na upendo baina yao.
Mama
Lwema aliwaomba wanawake wanaofunga kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa
Ramadhani wajitoe kufunga kwao kwa ajili ya maombi maalum ya kuombea
amani na watoto kwani hivi sasa vijana wengi wanaomaliza vyuo hawana ajira, shule haziendi sawa na wanaopata machungu ya haya yote ni wanawake
Post a Comment