Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MFUNGAJI BORA KAGAME ASAINI MIAKA MIWILI JIONI HII SIMBA SC



Dole gumba; Tambwe akikandamiza dole gumba

Na Mahmoud Zubeiry, wa Bin Zubeiry
 
MFUNGAJI bora wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati mwaka huu, Amisi Tambwe wa Vital’O ya Burundi jioni hii amesaini Mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba SC ya Dar es Salaam.
Tambwe amesaini ofisini kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe mbele ya Katibu wa timu hiyo, Evodius Mtawala. 
Tambwe ameiongoza Vital’O kutwaa taji la kwanza la Kagame mwaka huu katika michuano iliyofanyika nchini Sudan na pia akiibuka mfungaji bora wa mashindano hayo kwa mabao yake sita.
Dili limetimia; Hans Poppe akiwa ameshikana mikono na Tambwe baada ya kusaini

Na huyo pia ndiye mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Burundi na mshambuliaji chaguo la kwanza katika timu ya taifa ya nchi hiyo, Int’hamba Murugamba, ambaye anamfanya mchezaji wa Yanga, Didier Kavumbangu awe nje ya kikosi.  
Tambwe aliyefunga mabao 18 msimu uliopita wa Ligi Kuu ya Burundi, alitua mapema wiki hii kutoka kwao Bujumbura na baada ya kusaini, anarejea kujiunga na timu yake ya taifa kwa ajili ya mechi za CHAN.
Tambwe amewapiku mshambuliaji kutoka Sudan Kusini, Kon James kutoka klabu ya Al Nasir Juba ambaye anaendelea na majaribio.
Tambwe anakuwa mchezaji wa nne aliyejihakikishia kuwamo katika orodha ya wachezaji wa kigeni wa Simba, msimu ujao, wengine wakiwa ni Waganda kipa Abbel Dhaira, beki Samuel Ssenkoom na kiungo Mussa Mudde.

Dole gumba; Tambwe akikandamiza dole gumba 

Beki mwingine Mganda, Assumani Buyinza aliyekuja kutoka Vietnam pamoja na washambuliaji Felix Cuipoi kutoka DRC na Kon James kutoka Sudan Kusini wataendelea kugombea nafasi moja ya mwisho
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top