Na Swahili TV
Aliyekuwa
Waziri Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Edward Lowassa, amemsifia
Rais Jakaya Kikwete kuwa ameweza kuifanya Tanzania kupata
heshima katika ulingo wa kimataifa, aliyasema hayo wakati akihojiwa na
Swahili TV jijini Washington DC.
Alisema kitendo cha Rais wa Marekani Bwana Barack Obama kuja nchini na
viongozi mbalimbali wa mataifa makubwa kumeonyesha Rais Kikwete anakubalika.
“Ni
hivi karibuni tu Rais Xi Jinping wa China, Rais Obama na Rais mstaafu
wa Marekani George W.Bush walikuwa nchini Tanzania, hii inaonyesha
kuwa Tanzania iko juu katika medani za kimataifa” alisema Mheshimiwa
Lowassa.
Mheshimiwa Lowassa ambaye yuko nchini Marekani kwa ziara ya kikazi, aliongeza kwa kusema, Rais Kikwete anastahili pongezi sana kwa hilo kwani sio rahisi kwa viongozi wa mataifa makubwa kutembelea nchi zingine labda kama mko juu sana katika medani za kimataifa.
Pia
alisema Rais Kikwete amekuwa akihusishwa na utatuzi au ushauri wa
kutatua matatizo mbalimbali ya nchi zingine na pia ameanza kuishirikisha
Tanzania katika usimamizi wa amani katika nchi mbalimbali.
Tanzania
iliweka historia hivi karibuni kwa maraisi wawili wa Marekani kukutana
katika nchi moja kwa wakati mmoja, Rais Barack Obama na George W.Bush
walikutana jijini Dar es Salaam mwezi huu.
kwa habari zaidi tembelea Swahili TV Blog
Post a Comment