Spika
wa baraza la wakilishi Zanzibar Pandu ameir kificho amesema Baraza la
wakilishi liwe na Tahadhari sana kufanya maamuzi ambayo utekelezaji wake
umo katika mikono ya Serikali ili kuiepusha Serikali kuja kuingia
katika kitahanani kwa lile amblo kulitimizia Taifa mahitaji yake muhimu.
Hayo
ameyasema leo huko Baraza la wakilishi wakati alipokuwa
akitoa ufafanuzi kwa mwakilishi wa Kwamtipura CCM Hamza Hassan Juma
wakati alipokuwa amezuia kifungu kuipitisha Wizara ya Mifugo na Uvuvi
kwa kusema uagiziaji wa kuku kutoka Nnje uzuuliwe kwani una
uwasokosesha mapato wafugaji wa ndani na kuliua soko lao.
Amesema
si vyema kutoa maamuzi ya moja kwa moja kulilazimisha hilo kuzuia kuku
kutoka nje wasiletwe nchini bila ya kuwa na utafiti wa
kutosha utao bainisha wazi kuwa hawahitajiki kuku wa nje.
kutosha utao bainisha wazi kuwa hawahitajiki kuku wa nje.
“sivizuri
kuzuia fungu hili na kukusema kuku wasiagiziwe kutoka nje bali tuwachie
Serikali wakachunguze ukweli wa hilo na baadae watuleteeripoti,”alisema
Spika.
Aidha
ali sema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina wapenda sana wananchi
wake kuona kua wanafanikiwa katika uzalishaji kwani ndio
lengo la Serikali yao kujikwamua na umasikini na kujipatia kipato wawe makini kuliko kuchukuwa maamuzi ya haraka.
lengo la Serikali yao kujikwamua na umasikini na kujipatia kipato wawe makini kuliko kuchukuwa maamuzi ya haraka.
Post a Comment