Mama mmoja ambaye alidanganya kuhusu majukumu yake
katika mauaji ya halaiki nchini Rwanda, ili kupata hifadhi ya ukimbizi nchini
Marekani, amekuhumiwa kifungo cha miaka kumi gerezani.
Viongozi wa mashtaka wanasema kuwa Beatrice
Munyenyezi, 43, ambaye alikwenda nchini Marekani mwaka wa 1998, kwa wakati mmoja
alisimamia kituo kimoja cha ukaguzi ambako waathiriwa walichaguliwa ili kwenda
kunyongwa.
Mama huyo amepewa kifungo hicho kwa kutoa habari za
Baada ya kukamilisha hukumu yake, Bi Munyenyezi
atarejeshwa nchini Rwanda ambako anatarajiwa kufunguliwa mashtaka ya mauaji ya
halaiki.
Zaidi wa watu laki nane, wengi wao kutoka kwa kabila
la Watusti, ambao ndio wachache nchini Rwanda, waliuawa mwaka wa
1994.
Munyenyezi ni mshukiwa wa kwanza kuhukumiwa nchini
Marekani kuhusiana na mauaji hayo yaliyotokea nchini Rwanda.
Baada ya hukumu hiyo kutolewa, mama huyo alilia mbele
ya mahakama, mjini Concord katika jimbo la New Hampshire.
Wakati wa kesi hiyo, Jaji Judge Stephen McAuliffe
alisema Munyenyezi alikuwa amepata uraia wa Marekani kwa njia ya ulaghai na
udanganyifu.
Baada ya mauaji hayo kumalizika, alitorokea nchini
Kenya ambako alifanikiwa kupata watoto wawili.
Baaadaye alikwenda nchini Marekani kama mkimbizi na
alipata makao katika jimbo la Kaskazini Mashariki la New Hampshire, baada ya
kusaidiwa na mashirika ya kutoa misaada.
Kisha alijiunga na chuo kikuu huku akifanya kazi
katika ofisi moja ya serikali.
Lakini mashahidi waliliambia mahakama hiyo kuwa mama
huyo alikuwa kamanda wa kituo kimoja cha ukaguzi mjini Butare Kusini mwa Rwanda,
ambako Watutsi wengi waliuawa.
Mawakili wake wanasema wanapanga kukata
rufaa.
Mume wake Arsene Shalom Ntahobali na mamake
wanatumikia kifungo cha maisha nchini Rwanda baada ya kupatikana na hatia ya
kuhusika na mauaji ya halaiki nchini Rwanda.
Post a Comment