Mwenyekiti wa Kitongoji cha
Kwemakumbi katika kijiji cha Kireguru wilaya ya Kilindi mkoani Tanga,
Hamza Rajabu Ngaramilo(56), leo amehukumiwa kifungo cha miaka minne
jela baada ya kupatikana na hatia ya kuomba na kupokea rushwa ili kugawa
ardhi kwa wahamiajiwageni kijijini hapo.
Akisoma
hukumu katika kesi nambari 113/12 iliyosomwa kwa mara ya kwanza Mei 7,
mwaka jana, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Handeni
mkoani humo Patrick Maligana, amesema kuwa ameridhika na ushahidi
uliotolewa na upande wa Serikali na hivyo anamtia hatiani mtuhumiwa huyo
kama alivyoshtakiwa katika kosa hilo.
Awali
Mwendesha Mashtaka wa (TAKUKURU) wilayani Handeni Bw. George Magoti,
alidai kuwa Septemba mwaka 2012 siku na wakati usiofahamika, mtuhumiwa
akiwa ni mtumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilindi kwa nafasi ya
Mwenyekiti wa kitongoji cha Kwemakumbi katika Kijiji cha Kireguru,
aliomba na kupokea rushwa ya shilingi 300,000.
Mtuhumiwa
huyo wakati huo akiwa na umri wa miaka 55, alipokea fedha hizo kutoka
kwa Gwandu Gaheri Langida na Kesi Safari Tlatlab ambao wote ni wahamiaji
wageni kutoka katika kijiji cha Mang’ola Barazani wilaya ya Karatu
mkoani Arusha ili awapatie ardhi kwa ajili ya kilimo.
Mwendesha
Mashitaka huyo alisema, mtuhumiwa huyo aligawa ardhi hiyo yenye ukubwa
wa ekari 40 jambo ambalo alisema ni kinyume cha sheria za ugawaji wa
ardhi vijijini.
Bw.Magoti
ameifafanulia mahakama hiyo kuwa, kwa mujibu wa taratibu za ugawaji wa
ardhi vijijini, Mwenyekiti wa kitongoji ama kijiji anao uwezo wa kugawa
ardhi isiyozidi ekari kumi kwa malipo ya shilingi 5,000 kwa mwanakijiji
mkazi na shilingi 10,000 kwa mwanakijiji mhamiaji tofauti na alivyofanya
mtuhumiwa kwa wahamiaji hao wageni.
Mwendesha
Mashtaka huyo wa TAKUKURU ameiomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa
mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa Wenyeviti wengine wanaokiuka utaratibu wa
ugawaji wa ardhi vijijini na kuwafanya wananchi kutoa fedha nyingi
kinyume na utaratibu kama ilivyo kwa mtuhumiwa huyo kitendo
kinachotafsiriwa kuwa ni rushwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
Akitoa
hukumu hiyo, Hakimu Maligana alisema kuwa ameridhika na ushahidi
uliotolewa mahakamani hapo na kwa kuzingatia umri mkubwa wa mtuhumiwa
huyo, anamhukumu kulipa faini ya shilingi 150,000 ama kwenda jela miaka
minne kama atashindwa kulipa faini hiyo.Lakini ili
kujua kwamba maisha ni magumu hasa huko vijijini waliopo Wanzania wengi,
Mtumiwa huyo alipelekwa Gerezani kuanza kifungo cha miaka minne jela
baada ya kushindwa kulipa faini hiyo ya shilingi 150,000 na hivyo kuanza
maisha mapya ya kifungwa Gerezani.
Hata
hivyo pamoja na Mshitakiwa huyo kubadilishwa jina na kuitwa mfungwa,
lakini Hakimu amesema anaweza kutoka Gerezani wakati wowote endapo
atatokea ndugu ama rafiki wa kumlipia faini hiyo na stakabadhi ya malipo
ya serikali ikapelekwa kwa Mkuu wa Gereza la Handeni. Ardhi husika
itaendelea kubaki mikononi mwa walalamikaji
Post a Comment