JESHI
LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
11
Julai, 2013
Taarifa
kwa Vyombo vya Habari
Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linaadhimisha siku ya mashujaa kila
tarehe 25 Julai, ikiwa ni sehemu ya kuwakumbuka mashujaa waliopigana na
kushinda vita ya Kagera mwaka 1978/1979.
Maadhimisho
hayo hufanyika mara moja kwa mwaka, na mwaka huu yatafanyika tarehe 25 Julai
2013 katika mkoa wa Kagera wilaya ya Bukoba kwenye makaburi ya mashujaa yaliyopo
Kaboya.
Mgeni
rasmi katika maadhimisho hayo atakuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. JAKAYA MRISHO KIKWETE.
Sambamba
na mgeni rasmi, watakuwepo viongozi waandamizi wa Serikali, vyombo vya Ulinzi na
Usalama, vyama vya siasa, taasisi za dini na taasisi mbalimbali za
kiraia.
Vyombo
vya habari
vinaalikwa kushiriki katika maadhimisho hayo ambayo ni muhimu kwa
Taifa.
Imetolewa
na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao
Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP
9203, Simu: 0764742161
Email:
ulinzimagazine@yahoo.co.uk



Post a Comment