Na Prince Akbar, - Bin Zubeiry
SIMBA
SC ya Dar es Salaam, imemaliza ziara yake ya mikoani kujiandaa na msimu
kwa sare ya 1-1 na Polisi Mara kwenye Uwanja wa Karume, Musoma mkoani
Mara jioni hii.
Simba inayofundishwa na kocha mzawa, Alhaj Abadallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ ilikaribia kushinda leo kama si wenyeji kupata bao la kusawazisha dakika za lala salama.
Katika mchezo huo, uliovuta mashabiki wengi uwanjani, bao la Simba SC lilifungwa na mshambuliaji Marcel Kaheza kipindi cha kwanza kufuatia kazi nzuri ya mshambuliaji mpya, Zahor Pazi, aliyekuwa mwiba kwa ngome ya Maafande wa Mara leo.

Huo ulikuwa mchezo wa nne kwa Simba SC katika ziara yake hiyo, baada ya awali kuzifunga Rhino FC ya Tabora 3-1, kombaini ya Katavi 2-1 mkoani Katavi na Kahama United 1-0 mkoani Shinyanga.
Katika mchezo wa leo, kikosi cha Simba SC kilikuwa; Andrew Ntala, Haruna Shamte/Nassor Masoud ‘Chollo’, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Hassan Isihaka/Mussa Mude, Rahim Omar/Samuel Ssenkoom, William Lucian ‘Gallas’, Marcel Kaheza/Christopher Edward, Felix Cuipoi/Jonas Mkude, Zahor Pazi, Sino Augustino/Betram Mombei na Ramadhan Singano ‘Messi’.
Simba SC sasa inatarajiwa kurejea Dar es Salaam kwa ajili ya mechi na URA ya Uganda Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
Post a Comment