 |
| Naibu
Waziri wa Wizara ya Kilimo na Maliasili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
Mhe. Mtumwa Kheir Mbarak akihutubia wakati wa sherehe fupi za ufunguzi wa ofisi
hizo za Tanzania Horticultural Association (TAHA) |
 |
| Mkurugenzi wa TAHA, Bi Jacqueline Mkindi akisema neno
la ufunguzi kwa Mh. Mtumwa
Kheir Mbarak na wageni
waharikwa wakati
wa sherehe hizo za ufunguzi wa Ofisi za
TAHA-Zanzibar |
 |
| Moja ya mashamba darasa ya TAHA yaliyopo eneo la Donge,
Wilaya ya Kaskazini Unguja. |
 |
| Wakulima wanaojishughulisha na kilimo cha Mazao ya
horticulture wakiwa katika moja ya Warsha zilizoandaliwa na TAHA masaa machache
kabla ya ufunguzi wa ofisi hizo kisiwani
hapo. |
 |
| Baadhi tu ya pilipili bora zinazolimwa na wakulima
wanachama wa TAHA, mazao haya yenye afya ni matokeo ya elimu za kilimo bora
zinazotolewa na wataalamu wa TAHA visiwani
humo. |
 |
| Hili ni soko la Darajani Zanzibar, ni baadhi tu ya
maeneo ambayo bidhaa za wakulima wa horticulture Zanzibar upelekwa na kuuzwa kwa
ajili ya kukizi haja za soko la ndani. |
 |
| Mkurugenzi wa TAHA akiteta Jambo na Mtaalamu wake kwa
upande wa Visiwani Mzee Biwi wakati alipotembelea moja ya mashamba ya tikiti
maji ya wakulima ambao ni wanachama wa
TAHA. |
 |
| Wataalamu kutoka Finland ambao ndio wawezeshaji wa
shughuli za TAHA Zanzibar wakitazama moja ya shamba la Matikiti maji la moja ya
vikundi wanachama wa TAHA. |
Ukiwa na swali hoja na maoni ingia hapa uwasiliane nao
leo TAHA
Taasisi kilele ya TAHA inayoundwa na wakulima
wanaojishughulisha na kilimo cha 'horticulture' nchini Tanzania hatimaye
imefungua rasmi ofisi zake kuu katika visiwa vyenye marashi ya karafuu Zanzibar.
Ufunguzi wa ofisi hizo zilizo mtaa wa Kikwajuni kwenye Jengo la mfuko wa
barabara ulitanguliwa na ziara fupi ya kutembelea maeneo ambayo Taasisi hiyo
imeanzisha mashamba darasa na kusajili vikundi vya wakulima ili waweze kufaidika
kwa karibu zaidi na ushauri wa kiufundi katika masuala ya kilimo cha
'horticulture' hali kadhalika masoko ya kuuza bidhaa zao ndani na nje ya
nchi.
Via Demashonews
Post a Comment