Na Jennifer Chamila,MAELEZO.TAASISI
ya Automobile Association Tanzania (AAT) imetoa tuzo kwa waandishi wa
habari kutoka katika vyombo vya mbalimbali vya habari walio shiriki
katika kutoa habari kwa wananchi kuhusu mafunzo yalio tolewa kwa
waendesha bajaji na pikipiki 2500 kuhusu matumizi salama ya barabara.
Tuzo
hizo zimetolewa leo pamoja fedha taslimu na Rais wa taasisi hiyo
Bw.Nizar Jivan katika sherehe fupi ilio fanyika ukumbi wa Idara ya
Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam,Waandishi wa habari kutoka vyombo
mbalimbali vya habari wamewaza kujinyakulia tuzo hizo.
Rais huyo
alitoa tuzo hizo kwa waandishi na watu waliosaidia kukamilisha
mafunzo hayo, ambapo miongoni mwao ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari
Maelezo Bw.Assa Mwambene, ambaye tuzo yake ilikabidhiwa kwa Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara hiyo, Zamaradi Kawawa.
Wengine
waliopata tuzo hizo ni Mohamed Ugassa kutoka gazeti la The
Guardian,Freginia Ole Swai kutoka ITV,Fred Mwanjara wa Channel Ten,Elias
Shamt wa TBC,Miguel Suleiman wa Citizen,Nasongelya Kilyanga wa Daily
News,Khadija Mussa wa gazeti wa Uhuru,Zainabu Malongo kutoka
Mwananchi,Hadja Hamis kutoka Mtanzania,Abas Yusuph mwandishi wa
kujitegemea,Judica Benedict wa The Guardian.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika sherehe hiyo Bw.Nizar amesema
kuwa,anawashukuru waandishi wa habari kwa kusaidia kutoa habari kwa
wananchi juu ya mafunzo hayo yalio husisha matumizi salama ya barabara
na jinsi ya kuepusha ajali za barabarani.
Vilevile taasisi hiyo imeitaka Serikali kuweka mikakati madhubuti ambayo itarahisisha kupambana na matumizi mabaya ya barabara.
“Serikali
ihakikishe bodaboda zote zipewe namba maalumu ili iwe rahisi huzitambua
pindi uhalifu utakapotokea kama ilivyo kwa teksi,” alisema Jivan.
Naye
mmoja wa waandishi wa habari aliyejinyakulia tuzo hizo , Ugassa kutoka
gazeti la The Guardian,ametoa wito kwa waandishi wa habari kuzidisha
uhamasishaji dhidi ya matumizi bora ya barabara na kulipa mkazo suala
hilo kama wafanyavyo katika masuala mengine kama vile Ukimwi.
Credit: Mafoto blog
Post a Comment