Alisema wafanyabiashara hao ni pamoja na wale
wenye ulemavu wa viungo na kwamba zoezi lina lengo la kuendeleza Jiji la Dar es
Salaam kuwa katika hali ya usafi.
Aidha, alisema ombaomba wote waliozagaa katikati
ya mitaa ya Jiji watakusanywa na kurudishwa makwao.
Sadik aliliambia gazeti hili jana kuwa uchunguzi
uliofanywa na ofisi yake, umegundua kuwa ombaomba asilimia 90 wanatoka nje ya
mkoa wa Dar es Saalam na asilimia 10 ni wa jijini ambao wanandugu wenye
uwezo.
“Tumeamua kuwarudisha ombaomba wote vijijini
kwao," alisema.
Aliongeza kuwa wamachinga wanaofanyabiashara
katika maeneo yasiyo rasmi watapelekwa kwenye masoko rasmi waliyopangiwa.
Alisema magari kwa ajili ya kuwasambaza wamachinga
wanaofanyabiashara za vyakula na mbogamboga barabarani watapelekwa kwenye masoko
ya vyakula, na wale wa bidhaa za madukani watatakiwa kukodisha fremu.
Alisema ofisi yake imeandaa kikosi cha askari wa
jiji na magari yatakayobeba bidhaa za machinga hao kwenye masoko
waliyopangiwa.
Sadik alisema kuwa lengo la zoezi hilo ni kuliweka
jiji la Dar es Salaam katika hali ya usafi na kufanana na majiji mengine duniani
yaliyokaa kibiashara.
Alisema wageni kutoka nje ya nchi wana nia yakuja
kuwekeza jijini na fursa hizo zipo kwa lengo la kuwanufaisha wananchi wote.
Uchunguzi uliofanywa na NIPASHE umegundua kuwa
baada ya ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama, Jiji la Dar es Salaam
liliendelea kuwa katika hali yake ya uchafu baada ya wafanyabiashara hao kurudi
kwa staili ya kuweka meza ndogo na kuuza vitu vidogovidogo, wakati wanaouza nguo
huanza kazi yao majira ya saa 11 jioni.
Maeneo ambayo NIPASHE ilishuhudia biashara hizo
zikiendelea kama kawaida ni Mwenge, Mabibo Posta na
Ubungo.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
Post a Comment