Naibu
Waziri Angellah Jasmine Kairuki akizungumza katika hafla ya uzinduzi
rasmi wa huduma ya mpya ya kidijitali za Wakala wa Usajili Ufilisi na
Udhamini (RITA) ambazo zitawawezesha wananchi wote wenye simu za mkononi
na mtandano kupata huduma mbali mbali za RITA kwa kutumia simu zao za
mikononi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Push Media Mobile, Freddie Manento akifafanua jambo katika
wakati wa uzinduzi wa huduma ya mpya ya kidijitali za Wakala wa Usajili
Ufilisi na Udhamini (RITA) ambazo zitawawezesha wananchi wote wenye simu
za mkononi na mtandano kupata huduma mbali mbali za RITA kwa kutumia
simu zao za mikononi. kulia ni Naibu Waziri Angellah Jasmine Kairuki na
kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Phillip Saliboko.
====== ==========
NAIBU
Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Angellah Kairuki amezindua
huduma ya mpya ya kidijitali za Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini
(RITA) ambazo zitawawezesha wananchi wote wenye simu za mkononi na
mtandano kupata huduma mbali mbali za RITA kwa kutumia simu zao za
mikononi.
Katika
huduma hiyo, wananchi wataweza kupata huduma zote zinazotolwa na RITA
kwa kuchagua kipengele anachotaka baada ya kutuma neno RITA kwenda namba
15584 na kupokea muongozo utakaomwezesha kujua utaratibu wa kusajili
kizazi au kifo kilichotokea hospitali na kwengine.
Pia
wanaweza kupata taraifa zao mbali mali kwa kutembelea tovuti ya wakala
hao, www.rita.go.tz, kwa kujiunga na mtandao wa kijamii wa www.facebook.com/ritatanzania na www.twitter.com/ritatanzania.
Akizungumza
katika uzinduzi huo, Waziri Kairuki alisema kuwa huduma hiyo itapunguza
msongamano wa wananchi kujua taarifa mbali mbali za vizazi na vifo na
nyinginezo zinaztotolwa na wakala hao.
Waziri
Kairuki alisema kuwa huduma hiyo ni kwa nchi nzima na kuipongeza RITA
kwa kushirikiana na Kampuni ya Push Media Mobile kwa kutengeneza huduma
hiyo yenye ubora wa hali ya juu.
“Huduma
hii ni muhimu sana kwa wananchi na itasaidia kwa kiasi kikubwa
kupunguza gharama za kusafiri umbali mrefu ili kupata taarifa hizo, sasa
taarifa utazipata kiganjani, tena kwa kutumia simu yako ya mkononi, ni
jambo la faraja na la kujivunia,” alisema Waziri Kairuki.
Alisema
kuwa Wizara yao ina mpango wa kuanzisha utaratibu ambao utaongeza kasi
ya usajili wa wananchi kwa wakala hao ambapo mwananchi hataweza kupata
kazi mpaka awe na cheti cha kuzaliwa. Pia hata kwa watu wanaotaka kupata
leseni za biashara, kujiunga na shule na shughuli nyingine mbali mbali
watalazima kuwa na cheti cha kuzaliwa.
Afisa
Mtendaji Kuu wa RITA, Phillip Saliboko alisema kuwa wameamua kujiunga
digitali ili kwenda na wakati na mpango wao mkubwa ni kupanua wigo wa
huduma zao kwa kaya zote.
“Tunataka
kuwa karibu zaidi na kushirikiana na umma, kwa kutumia tovuti, mitandao
ya kijamii na simu za mkononi kama njia ya kuwasiliana na kusambaza
taarifa muhimu kwa wananchi, hii itaturahisishia hata sisi kujua ufanisi
wa shughuli zetu na kukabiliana na changamoto mbali mbali,” alisema
Saliboko.
Saliboko
alisema kuwa kutokana na ongezeko la watumiaji wa intaneti, mitandao ya
kijamii na simu za mkononi, RITA iko tayari kwenda sambamba na
mabadiliko hayo na kutoa jukwaa la mawasiliano baina yao na wananchi.
Post a Comment