Mmoja wa wafanyakazi wa
Kampuni ya Jambo Freight Forwarder Bibi Vanessa Gwau kushoto akielezea jambo kwa
mwandishi wa habari wakati wa hafla ya kupokea mabomba yatakayotumika
kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadio Dar es Salaam. Jambo Freight ndiyo kampuni
iliyopewa zabuni ya kupakua shehena hiyo.
Balozi wa Jamhuri ya Watu
wa China Balozi Lu Youging katikati akifafanua jambo,kushoto ni Waziri wa
Nishati na Madini Prosefa Sospeter Muhongo,kutoka kulia Ms Wang Fang kutota
Ubalozi wa China anayemfuatia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sadick Meck
Sadick.
Waziri Mkuu Mheshimiwa
Mizengo Pinda akiwasili katika eneo la Bandari ya Dar es Salaam tayari kwa
kuzindua rasmi upokeaji wa shehena ya mabomba yatakayotumika katika ujenzi wa
mradi wa kusafirisha Gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mheshimiwa
Mizengo Pinda katika akibadishana jambo na Waziri wa Nishati na Madini Prosefa
Sospeter Muhongo aliyekaa kushoto,Kulia ni Balozi wa China nchini Tanzania
Balozi Lu Youging wakati wa hafla ya kuzindua kupokea shehena ya mabomba kwa
ajili ya mradi wa kusafirisha Gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mheshimiwa
Mizengo Pinda akishuhudia Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Balozi Lu Youging
alipokuwa akimalizia kufunua kitamba kama ishara ya uzinduzi rasmi wa upakeaji
wa mabomba ya Gesi.
Pichani mafundi wakiwa
katika zoezi la kupakua mabomba kutoka katika meli na kupakia kwenye Lori tayari
kwa safari ya Mtwara.
Waziri Mkuu Mheshimiwa
Mizengo Pinda akizungumza mara baada ya kuzindua rasmi upokeaji wa mabomba ya
gesi tayari kwa kusafishwa hadi Mtwara.PICHA ZOTE
NA FRANK SHIJA - MAELEZO
Na Frank Shija -
Maelezo
Serikali imewatoa hofu
wananchi wa Mtwara kuhusu kunufaika kwao na gesi asilia iliyopatikana katika
maeneo yao.
Hayo yamebainishwa na
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda alipokuwa akizindua
rasmi upokeaji wa shehena ya mabonba ya gezi kwa ajili ya mradi wa bomba la
kusafirishia Gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam mwisho ni wiki jijini Dare se
Salaam.
Pinda amesema kuwa wananchi
wa watanzania watanufainaka na mradi huo hasa hasa wakazi wa Mtwara kwakuwa
vijana wengi watapata ajira wakati na baada ya kukamilika kwa ujenzi wa bomba
hilo kwakuwa viwanda mbalimbali vitajengwa mkoani Mtwara kikiwemo kiwanda cha
Saruji ambacho ujenzi wake umekwisha anza.
“Ndugu zangu wana Mtwara ni
waambe tu wakati wa kunufaina na rasilimali ya Gesi sasa umefika,niseme tu mradi
huu utakapokamilika fursa mbalimbali zitafunguka ikiwemo ajira kwa wakazi wa
Mtwara”. Alisema Pinda.
Kwa upande wake Balozi wa
Jamhuri ya Watu wa Chini hapa nchini Balozi Lu Youging amesema kuwa Tanzania
itanufaika na mradi huu na kukua kiuchumi kwakuwa itapunguza kwa kiasi kikubwa
matumizi katika nishati na badala yake itazalisha nishati
yakutosha.
Balozi huyo aliongeza kuwa
kutpitia mradi huu Tanzania itaondokana na kuwa tegemezi katika shughuli zake za
maendeleo kwa kuwa kuna hazina ya kutosha ya gesi asilia na itawanufaisha
watanzania wenyewe na si vinginevyo.
Jumla ya mabomba 3400
yamepokelewa katika awamu ya kwanza ambapo awamu ya pili itapokelewa shehena
yenye mabonmba 4600 katika bandari ya Mtwara.Inakadiriwa kuwa jumla ya shehena
12 zitatumika mpaka mradi utakapokuwa
umekamilika.
CREDITS: MICHUZI MATUKIO BLOG
Post a Comment