Na Azimio
Sote
SERIKALI imesema
msimamo wa serikali kuanzisha tozo ya kodi katika laini za simu hautabadilika
kutokana na ulazima wa kupata fedha kwa ajili ya kuunganisha umeme maeneo ya
vijijini ambako bado watu wengi wanaishi bila
umeme.
Hayo yalisemwa
jana na Waziri Mkuu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo
Pinda alipokuwa akihutubia wananchi na viongozi mbalimbali kwenye mkutano
uliofanyika katika viunga vya Halmashauri ya Manispaa ya
Songea.
Mizengo Pinda
alisema kuwa kodi ya laini imewekwa mahususi ili kukusanya fedha ambazo
zitatumika katika kuunganisha umeme kwenye maeneo mengi hususani ya vijijini
ambayo kwa sasa hayana umeme jambo ambalo alisema linakwamisha
jitihada za wananchi kujiletea maendeleo ambapo alisema kila mtumia laini ya
simu atapaswa kulipa kodi ya shilingi elfu moja kwa
mwezi.
Aidha, Pinda
aliwashangaa watu wanaopinga tozo hii akidai kuwa ni ndogo kwa kuwa ni sawa na
kutoza shilingi therathini kwa siku kiasi ambacho kiko chini sana ikilinganishwa
na matumizi ya kawaida kama kuvuta sigara ambapo alisema kuwa suala la tozo
katika laini linatokana na shinikizo la wabunge kuitaka serikali itafute vyanzo
vya mapato vitakavyotumika kusambazia umeme maeneo ya
vijijini.
“Serikali
ilielekezwa bungeni kuwa itafute vyanzo vyoyote vile kupata umeme
vijijini…tukakaa tukaangalia tukaona ni vema wananchi wachangie shilingi 1000
katika kila laini kiasi ambacho kitaiwezesha serikali kukusanya kiasi cha
shilingi bilioni 160 kwa ajili ya umeme vijijini”, alisema
Pinda.
Hivyo, waziri
Pinda akasisitiza kuwa serikali itaendelea kukusanya kodi katika laini za simu
hata kama wananchi watalalamika lakini mwishoni lazima watalazimika kuelewa
tu.
Awali Naibu
waziri wa Nishati na Madini Steven Maselle alipata wakati mgumu alipojaribu
kuwaeleza wananchi haja ya kukusanya kodi kwa kila laini ya simu ambapo wananchi
waliguna kwa nguvu kuashiria kuwa hawakubaliani na kauli hiyo jambo lililomfanya
Waziri Pinda alitolee ufafanuzi zaidi.
Uhusiano wa
Tanzania na Malawi.
Akizungumzia
suala la uhusiano wa Tanzania na Malawi Waziri Mkuu Pinda alisema kuwa kimsingi
serikali ya Tanzania haina nia wala sababu ya kuingia vitani na Serikali ya
Malawi kwa kuwa suala lililopo linaweza kupata ufumbuzi bila ya kuingia vitani
ambapo alisema kuwa kwa sasa suala hili limepelekwa katika Jumuiya ya Nchi za
Kusini Mwa Afrika (SADDC) kwa usuluhishi ambako Marais wawili wastaafu wamepewa
jukumu la usuluhishi wa tatizo hili.
Kwa upande
mwingine Waziri Pinda alisema ikiwa SADDC hawatafanikiwa kupata suluhisho na
serikali ya Malawi ikaamua kwenda katika mahakama za kimataifa Tanzania iko
tayari kwenda kujitetea kwa vile haioni wapi
ilipoteleza.
“Hata wakipeleka
suala hili katika mahakama ya Kimataifa tuko tayari kupeleka wanasheria wetu
waliobobea tutakwenda kujieleza vizuri kwani hatuoni tulipokosea,” alisema
Pinda.
Hata hivyo
alionya kuwa ikiwa atatokea mtu, kwa sababu zake mwenyewe, akaamua kuivamia
Tanzania nchi haitakuwa na budi kujitetea kwa kupambana naye kwa vile uwezo wa
kupambana upo ambapo alitolea mfano wa kilichomkuta Idd Amin wa
Uganda.
Vilevile Mizengo
Pinda alisema kuwa kuna tatizo la miundombinu ya mawasiliano eneo la mwambao mwa
ziwa Nyasa ambako wananchi wanakosa taarifa za vyombo vya habari vya Tanzania na
badala yake wanapata kiurahisi zaidi taarifa za Malawi fursa ambayo Pinda
alisema inaweza ikawa inatumika vibaya kwa kuwapotosha wananchi wanaoishi
pembezoni mwa ziwa Nyasa ambapo aliahidi kulipatia ufumbuzi tatizo hili kwa
kufunga mitambo itakayowezesha wananchi hawa kupata taarifa za habari kama
kawaida.
Suala la
Ujangili
Waziri Mkuu
Mizengo Pinda alisema kuwa serikali inasikitishwa na tabia ya watu kujihusisha
na ujangili katika mbuga za taifa ambapo alisema hayo yanafanyika zaidi mkoani
Ruvuma katika mbuga ya wanyama ya Selous ambapo aliwashangaa watu wanaojua uwepo
wa ujangili na wanawajua watu wanaofanya ujangili lakini wanasema hakuna
ujangili wakati wanyama wanazidi kuangamia.
Ndipo Pinda
akasema kuwa serikali imejipanga kuhakikisha kuwa majangili yanasakwa popote
yalipo, kunakamata na kufikishwa katika vyombo vya sheria ambapo alisema kuwa
kwa sasa serikali imeanzisha oparesheni uhai inayolenga kunusuru viumbe hai
vyote na inakusudia pia kupambana na majangili na ujangili nchini ingawa alikiri
kuwa hadi sasa oparesheni hii bado haijaanza kufanya
kazi.
Vilevile Waziri
Pinda alikemea tabia ya vyombo vinavyohusika na kutoa silaha kwa wamiliki
binafsi ambapo alivitaka kuhakikisha kuwa silaha zinatolewa kwa sababu na idadi
maalumu ili kupunguza idadi ya watu wenye kumiliki silaha ambazo baadhi huishia
kutumika katika ujangili.
Post a Comment