Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Idara ya uhamiaji wakati alipowasili
kwenye jengo la Idara hiyo mjini Songea kuweka jiwe la msingi akiwa katika ziara
ya mkoa wa Ruvuma Julai 20, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
akikagua mabwawa ya kufugia samaki wakati alipotembelea Kituo cha Maendeleo ya
Ufugaji Samaki cha Ruhila kilichopo mjini Songea. Alikuwa katika ziara ya mkoa
wa Ruvuma Julai 20, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
akitazama chakula cha samaki wakati alipotembelea Kituo cha Maendeleo ya Ufugaji
wa Samaki cha Ruhila kilichopo Songea Mjini akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma
Julai 20, 2013. Wapili kulia ni mkewe, Mama Tunu Pinda na Kushoto ni Mkuu wa
Mkoa wa Ruvuma, Thabit Mwambungu.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
akitazama moja ya magari ya mafunzo yanayotumika katika Chuo cha Mafunzo ya
Ufundi Tanzania (VETA) cha Songea wakati alipokizindua,Julai 20, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
na Mkewe Tunu (wapili kuhoto) wakitazama vyakula na vifaa mbalimbali vya jikoni
katika maonyesho ya kozi zinazofndishwa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Tanzania
(VETA) cha Songea wakati alipokizindua Julai 2013.
Wairi Mkuu, Mizengo Pinda
na mkewe Tunu wakisalimiana na madiwani wa Manispaa ya Songea wakati Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda alipohutubia mkutano wa hadhara mjini Songea akiwa kayia
ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 20, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
na mkewe Tunu (kushoto kwake) wakitazama ngoma ya wanawake wa Songea kabla ya
kuhutubia mkutano wa hadhara mjini Songea Julai 20, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
akisalimiana na wanafnzi wa Shule ya Sekondari ya Songea Girls baada ya
kuhutubia mkutano wa hadhara mjini Songea Julai 20, 2013. Alikuwa katika ziara
ya mkoa wa Ruvuma.
Baadhi ya Waislam
walioalikwa katika futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye
Ikulu ndogo ya Songea wakishiriki katika futari hiyo Julai 20, 2013.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama
Tunu Pinda (wapili kulia) akizungumza na baadhi ya wanawake walioshiriki katika
futari ambayo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliwaandalia baadhi ya Waislam wa
Songea Julai 20, 2013. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Post a Comment