Zoezi la uchukuaji alama kwa vidole na kupiga picha kwa ajili ya vitambulisho
vya Taifa, limeaza kwa wakazi wa Manispaa ya Temeke, jijini Dar es
Salaam.
Kwa mujibu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), zoezi hilo limeaza na kanda ya kwanza katika manispaa hiyo itakayohusisha mitaa ya Kimbiji, Pemba Mnazi, Kigamboni, Vijibweni, Kibada, Mjimwema, Somangili, Kisarawe II, Tungi na Mitaa ya Mtoni Kijichi, Mgeninani na Misheni.
Nida imewaomba wakazi wa manispaa hiyo kujitokeza katika zoezi la ujazaji fomu za maombi ya vitambulisho hivyo na upigaji wa picha na uwekaji saini ya kielekroniki.
Afisa Habari wa Nida, Thomas William, alisema waombaji wanatakiwa kufika na vielelezo halisi vitakavyothibitishia uraia na umri wao.
“Vielelezo, ambavyo unatakiwa kuja navyo katika kituo ni vyeti vya kuzaliwa, pasipoti, vyeti vya elimu ya msingi na sekondari, kitambulisho cha bima ya afya, leseni ya udereva pamoja na kitambulisho cha kupiga kura,” alisema.

CHANZO: NIPASHE
Post a Comment