Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

ABOUD AKUTA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA NA KUWAPA MAAGIZO MAZITO

               
  
01 2e7dc
Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohd akizungumza na wawakilishi wa vyama vya siasa Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar juu ya suala zima la uboreshaji Sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Khadija Khamis na Amina Shaibu wa Habari Maelezo Zanzibar.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imewataka viongozi wa vyama vya siasa kushirikiana na kutoa mchango wao wa hali na mali katika kufanikisha sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar .
Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohammed Abuod Muhammed alipokutana na wawakilishi wa vyama vya siasa ofisini kwa ke Vuga.
Alisema kuwa Serikali imeamua kuzifanya sherehe hizo kuwa za aina yake na zinahitaji mchango wa kila mtu bila ya kuangalia itikadi ya vyama vya siasa ili kuonyesha uelewa wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa nchini.

 
"Mapinduzi yetu yanafikia nusu karne, tutafanya sherehe kubwa na tumeamua kuyashirikisha makundi yote kuanzia hatua za awali wakiwemo viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wafanya biasha, makampuni, taasisi binafsi, waandishi wa habari na makundi mengine ili kufanikisha sherehe hizo," alisema Waziri Aboud
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Mkamu wa pili wa Rais alidokeza kuwa Mgeni Rasmi katika Sherehe hizo atakuwa Rais wa Jamhuri ya watu wa China na wageni kutoka nchi za Afrika Mashariki, nchi wanachama wa SADC pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya ulaya pia wamealikwa kushiriki.
 
Aidha alisema katika shamrashara za sherehe hizo kutakuwa na ufunguzi wa miradi mbali mbali ya maendeleo, uwekaji wa mawe ya msingi, makongamano na utajengwa mnara maalumu wa miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar .
 
Nae katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamo wa pili wa Rais Dkt Khalid Salum Muhammed alisema kuwa katika kufanikisha sherehe hizo kumeandaliwa vazi rasmi siku ya kilele cha sherehe hizo yenye rangi za bendera ya Zanzibar.
 
Aliongeza kuwa vipindi maalum na picha za mafanikio ya Mapinduzi katika kipindi cha miaka 50 vitaendelea kuonyeshwa kupitia vyombo mbali mbali vya Serikali na binafsi na changamoto zilizojitokeza ili kuweza kukabiliana nazo katika kipindi chengine cha miaka 50 .

Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 yaliyoongozwa na Marehemu Abeid Amani Karume yatatimiza miaka 50 tarehe 12 Januari 2014 na kilele chake kitakuwa katika uwanja wa Amaan

MWISHO
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIB
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top