Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

BAADA YA KUWA NJE KWA DHAMANA, HENRY KILEWO ATOBOA SIRI NZITO



KWA watanzania wataka mabadiliko: jela siyo sehemu salama ya kuishi,wala haijawahi kuwa sehemu salama ya kuishi,wala haitakaa iwe sehemu salama ya kuishi pasipo tokea wajasiri na wazalendo kama mimi na wewe kwenda kuishi kwa hiari sehemu ambayo utawala dhaifu wa ccm unadhani ni kitisho cha kuzuia mabadiliko. 

Watawala wabovu kwenye nchi yetu hutumia jela kama kitisho cha kuzuia ukweli,ukiruhusu kitisho cha kuogopa jela utakuwa mwanamabadiliko kigeugeu na mnafiki mach
oni mwa umma.

Kitisho hiki kamwe sintokiruhusu mimi HENRY KILEWO hata kwa mtutu wa risasi za moto,japokuwa natambua athari za kukaa jela muda mrefu kama ambavyo shujaa wa dunia nelson mandela anavyopitia kwasasa, hii kwangu mimi ni sadaka tosha kwa taifa langu chama changu, familia yangu pamoja na ndugu jamaa na marafiki zangu.

Nionyo na funzo kwa watawala dhaifu kudhani wataweza kuzuia harakati hizi za mabadiliko kwa kuvitumia vyombo vya dola vibaya kama usalama wa taifa, jeshi la polisi, mahakama na hata magereza. 

Kamwe tusiruhusu kuwa wanyonge wala kukubali kuonewa kwani watatuzuia kwa muda, watatudhalilisha kwa muda na sikuogopa kukaa jela ila moyo wangu unasononeka pale nionapo saa ya ukombozi inachelewa. Ni muda tu, tutashinda.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top