Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

BALOZI MDOGO WA OMAN AJITAMBULISHA KWA WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI NA MICHEZO ZANZIBAR

 

01 (1)Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na michezo Said Ali Mbarouk, akimkaribisha Balozi Mgodogo wa Oman Salleh Suleiman Al-Harith Ofisini kwake alipofika kujitambulisha, huko Wizarani kwake kikwajuni Mjini Zanzibar 02 Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na michezo Said Ali Mbarouk akimpa maelezo Balozi Mgodogo wa Oman Salleh Suleiman Al-Harith juu ya mausiano ya kidugu ya Zanzibar na Oman (kulia ya waziri) 03 
Picha ya pamoja ya  Waziri wa Habari Utamduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk (alievaa koti),  Balozi mdogo wa Oman Salleh Suleiman  Al Harith na Naibu Waziri wa Habari, utamduni Utalii na Michezo Bihindi Hamad Khamis.
Na Mwanamgeni Amour na Amina Abeid (ZJMMC)             
 Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk ameshauri kuanzishwa Utalii wa uwenyeji kati ya watu wa Oman na Zanzibar ili kuendeleza ushirikiano wa muda mrefu kati ya nchi hizi mbili. Waziri Mbarouk ametoa ushauri huo alipokuwa akizungumza na Balozi mdogo wa Oman aliepo Zanzibar Salleh Suleiman Alharith huko Ofisini kwake Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.
 
Amesema Oman na Zanzibar zimekuwa na uhusino wa muda mrefu na wananchi wa nchi mbili hizi wamekuwa wakishirikiana katika nyanja mbali mbali za maendeleo na utamaduni hivyo kuanzishwa kwa utalii wa uwenyeji utaizidi kuimarisha uhusiano huo. “ Uhusiano wa kihistoria kati ya nchi mbili hizi umewezesha wananchi wa nchi hizi mbili  kudumisha mila na silka  zao kwa lugha zote mbili, Kiarabu na Kiswahili, ”alisema Waziri Saidi Ali Mbarouk. Aidha wazirihuyo amemshauri balozi mdogo wa Oman kuwahamasisha wawekezaji wa nchi hiyo kuja kuwekeza Zanzibar na kumueleza kwamba kumeandaliwa mazingira bora na vivutio vingi vya kuwekeza nchini.
 
Waziri Mbarouk ameiomba Serikali ya Oman kulifanyia matengenezo jengo la kihistoria la Beit el Ajab ambalo liliporomoka mapema mwaka huu  ili liweze kurejea katika hali yake ya kawaida. Aidha ameitaka nchi hiyo kusaidia vifaa vya kiwanda cha uchapaji cha Serikali kinachojengwa katika eneo la Maruhubi na kujengewa kiwanja cha Michezo katika Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Nae Balozi mdogo wa Oman amemshukuru Waziri Said Ali Mbarouk  na kumuahidi kuwa watayawasilisha  maombi yao katika Serikali ya Oman na ameeleza matumaini yake kwamba yatapatiwa ufumbuzi katika muda mfupi ujao kutokana na uhusiano na ushirikiano mkubwa uliopo kati  ya nchi hizi mbili. Amesema Oman wanajisikia fahari kusaidia ndugu zao wa Zanzibar na kusema kwamba imeweka milango wazi kwa wananchi wa pande hizi mbili  kujenga ushirikiano wa karibu zaidi na kusaidiana.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top