TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
Kila mwananchi wa Zanzibar ameshitushwa na kusikitishwa
na tukio la kumwagiwa tindikali kwa raia wawili wa Kiengereza usiku tareh 7
Agost 2013 huko katika maeneo ya Mji mkongwe Zanzibar yaliopo mahoteli mengi na
makazi ya wageni wanaotembele nchi yetu kutoka sehemu mbali mbali
duniani.
Chama Cha wananchi CUF kinalaani kwa nguvu zote tukio
hilo la kikatili la kuwamwagia tindi kwa wageni wetu hao,na kinalitaka Jeshi la
Polisi Zanzibar kufanya uchunguzi wakina na waharaka pamoja na kuhakikisha kuwa
wale wote waliohusika na tukio hilo la kikatili wanakamatwa na kufikishwa
katika vyombo vya sheria.
Matokeo haya ya kikatili ya kumwagiwa kwa watu tindi
kali yamekuwa yakishamiri siku hadi siku ndani ya visiwa vya Zanzibar,ambayo
yamekuwa yamewathiri watu kadhaa tena bila ya wahusika kuweza kupatikana na
kuchukuliwa hatuwa za kisheria kiasi ambacho sasa jamii ya wazanzibar imejengeka
katika hofu juu ya usalama wa maisha yao ya kila siku,Hii ni dalili mbaya kwa
Nchi ya Zanzibar kwani matukio haya ya tindikali yamekuwa yanaonekana kama ni
masuala ya kawaida jambo ambalo linatishia uchumi wa Visiwa
vyetu.
Kufanyiwa hujuma raia hao wakike wawili wa kigeni
kutoka nchini Uengereza kigeni ambao walikuwa Zanzibar kwa kazi za kujitolea
(valantia) kusomesha katika skuli za msingi (primary)
ni dhahiri kuwa Sekta muhimu inayotegemewa katika kukuza uchumi wa Zanzibar (utalii)inaweza kutetereka.
ni dhahiri kuwa Sekta muhimu inayotegemewa katika kukuza uchumi wa Zanzibar (utalii)inaweza kutetereka.
Chama cha wananchi CUF kinawataka wananchi wote wa
Zanzibar kutoa kila aina ya mashirikiano ya kuweza kufanikisha kukamatwa
wahalifu hao na hatimae kufikishwa katika sehemu husika.
Sambamba na hilo Chama cha wananchi CUF Kinawataka
Wanachi wote, Polisi jamii kutoa kila aina ya mashirikiano kwa Jeshi la Polisi
ili jeshi hilo liweze kukomesha kabisa vitendo vyote vya kihalifu ndani ya nchi
yetu, kwa lengo la kuiendeleza sifa ya asili ya zanzibar isemayo kuwa Zanzibar
ni njema atakae na aje…
Haki sawa kwa
wote.
Salim A
Biman
Mkurugenzi wa Haki za
Binaadamu, Habari, Uenezi, Mawasiliano na Umma



Post a Comment