Waziri
wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji
wa benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla
ya kukabidhi wodi ya wazazi iliyofanyiwa ukarabati na benki hiyo katika
Hospitali ya Rufaa Mbeya, Kitengo cha Huduma ya Akinamama na
Watoto-Meta. Hafla hiyo ilifanyika mjini Mbeya, mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akifafanua jambo wakati wa hafla hiyo.
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia), akipanda
mti wa kumbukumbu wakati wa hafla ya kukabidhi wodi ya wazazi iliyofanyiwa
ukarabati na benki hiyo katika Hospitali ya Rufaa Mbeya, Kitengo cha Huduma ya
Akinamama na Watoto-Meta. Hafla hiyo ilifanyika mjini Mbeya, mwishoni mwa
wiki.
Waziri
wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akipanda mti wa kumbukumbu katika
hospitali ya Rufaa ya Meta wakati wa hafla ya kukabidhi wodi ya wazazi
iliyofanyiwa ukarabati mkubwa na benki ya CRDB. Kulia ni Mkuu wa Wilaya
ya Mbeya, Dk. Norman Sigalla na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki
hiyo, Dk. Charles Kimei.
Waziri wa Uchukuzi, Dk.
Harrison Mwakyembe (katikati) akimwagilia mti wa kumbukumbu pamoja na
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei wakati benki hiyo
ilipokabidhi wodi ya wazazi katika
Hospitali ya Rufaa Mbeya, Kitengo cha Huduma ya Akinamama na Watoto-Meta.
Zoezi la upandaji miti likiendelea.
Waziri
wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe akikata utepe wakati wa kukabidhi
wodi ya wazazi katika Hospitali ya Rufaa Meta, ambayo imefanyiwa
ukarabati na benki ya CRDB. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki
mjini Mbeya. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dk. Charles
Kimei, kushoto ni Murugenzi wa tawi la Mbeya, Benson Mwakyusa na Mkuu wa
Wilaya ya Mbeya, Dk. Norman Sigalla.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa
benki ya CRDB, Tully Mwambapa akimkabidhi kasha la juisi, Salome
Zakaria, ambaye ni mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya
Rufaa Mbeya Kitengo cha Huduma ya Akinamama na Watoto-Meta, wakati wa hafla ya benki hiyo kukabidhi wodi ya wazazi iliyofanyika mjini Mbeya, mwishoni mwa wiki.
Pole mama, pokea zawadi.
Tucheze kwaito.
Mfanyakazi wa benki ya CRDB tawi la Viwawa, Mbozi, Beatrice Kyando akimwagilia maji mti wa kumbukumbu alioupanda.
Waziri
wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akipaka rangi wodi ya wazazi katika
hospitali ya Rufaa ya Meta, wakati wa hafla ya kukabidhi wodi hiyo kwa
uongozi wa hospitali hiyo baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa na benki
ya CRDB. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki mjini Mbeya.
Mke wa Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akiwafariji wagojwa waliolazwa katika wodi ya wazazi katika hospitali ya Rufaa ya Meta.
Mkurugenzi
Mtendaji wa benki hiyo, Dk. Charles Kimei wakati wa hafla iliyoandaliwa
na benki hiyo kwa ajili ya wadau na wateja wa benki hiyo iliyofanyika
mjini Mbeya.
Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza katika hafla hiyo.
Tucheze mduara
Wadau wakicheza Kwaito.
Post a Comment