
Mwakilishi wa timu ya KMKM ya unguja Said Mfaume akipokea jezi toka kwa Waziri wa habari,utalii na michezo Zanzibar Said Mbarouk tayari kabisa kwa kuanza kwa ligi kuu ya Grandmalt Zanzibar,Kulia ni meneja masoko wa GrandMalt Fimbo buttala na Rais wa ZFA Ravia Faina. (Na Mpiga Picha Wetu)
Mwakilishi wa timu ya Mafunzo ya pemba Khamis Ally akipokea jezi toka kwa Waziri wa habari,utalii na michezo Zanzibar Said Mbarouk tayari kabisa kwa kuanza kwa ligi kuu ya Grandmalt Zanzibar,Kulia ni meneja masoko wa GrandMalt Fimbo buttala na Rais wa ZFA, Ravia Faina.
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
KINYWAJI
kisicho na kilevi cha Grand Malt, walio wadhamini wa Ligi Kuu ya
Zanzibar maarufu kama ‘Grand Malt Premier League’ jana walikabidhi rasmi
vifaa kwa timu 12 zinazoshiriki ligi hiyo katika hafla iliyofanyika
hoteli ya Bwawani, mjini hapa.
Mbali
na kumwaga vifaa hivyo, Grand Malt pia wameamua kufanya kweli zaidi kwa
kuongeza udhamini wao kwa waamuzi na uendeshaji wa ligi, ambapo msimu
huu watatoa kiasi cha Sh milioni 200 kutoka Sh milioni 140 za msimu
uliopita.
Hafla
hiyo maalumu ya kukabidhi vifaa na kutangaza kiasi hicho kipya cha
uendeshaji wa ligi, ilihudhuriwa na viongozi na wanamichezo mbalimbali
wakiongozwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Saidi Ali Mbarouk.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Mbarouk alisema wamefurahishwa mno na Grand Malt kwa
kuongeza udhamini wao pamoja na kutoa vifaa bora vya michezo kwa timu
zote zishiriki.
“Tuna
uhakika sasa soka ndani ya Zanzibar itazidi kusonga mbele, ombi lenu
kwenu ZFA (Chama cha Soka Zanzibar), pamoja na wadau wote kutumia fursa
hii kuhakikisha tunafika kule tunakokutaka.
“Nawasifu
zaidi Grand Malt kwa kuendelea kudhamini Ligi Kuu ya Zanzibar nah ii
inadhihirisha tuko nao pamoja kwa mambo mengi, nasi pia tunapaswa
kuwaunga mkono kwa kutumia kinywaji chao,” alisema.
Mkurugenzi
wa Masoko wa Grand Malt, Kushillah Thomas naye alisema, kinywaji hicho
kitaendelea kushirikiana na watu wa Zanzibar katika kuhakikisha
wanafanikiwa kwenye malengo yao.
“Udhamini huu ni mwanzo tu na tunaamini utasaidia kwa kiwango kikubwa kufanikisha malengo ya soka ya Zanzibar,” alisema.
Viongozi
wa ZFA nao walikiri kufurahishwa na udhamini huo na kusema, wanaamini
Ligi Kuu ya Grand Malt msimu huu itakuwa na ushindani mkubwa zaidi.
KMKM ndio waliofanikiwa kutwaa ubingwa huo msimu uliopita, wakiwa ni mabingwa wa kwanza toka kuanza kwa udhamini wa Grand Malt.
Mbali
na KMKM timu nyingine zinazoshiriki ligi hiyo ni Fuoni, Chuoni, Polisi,
Malindi (Bandari), Zimamoto, Mafunzo, Jamhuri, Chipukizi, Kizimbani,
Mtende na Miembeni.
Kinywaji
cha Grand Malt kisicho na kilevi ndio walioingia mkataba wa kudhamini
ligi hiyo, hivyo kujulikana kama Ligi Kuu ya Grand Malt.




Post a Comment