Sheikh
Ponda akisisitiza jambo kwa waumini wa Kiislamu eneo la Uwanja wa
Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro, muda mfupi
kabla ya kudaiwa kujeruhiwa kwa risasi katika eneo la bega katika mwili
wake Augosti 10, mwaka
huu.
********
TUKIO la kujeruhiwa kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Sheikh Ponda Issa Ponda na kitu kinachodhaniwa kuwa ni risasi mkoani Morogoro kimeamsha hisia tofauti miongoni mwa watetezi wa haki za binadamu na taasisi mbalimbali za dini nchini Tanzania.
Watetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania kupitia kituo cha sheria na haki za binadamu Tanzania pamoja na kulaani tukio la kujeruhiwa kiongozi huyo wa taasisi ya kiisalam wamet
aka tume ya haki za binadamu na utawala bora nchini kufuatilia pia matukio mengine ambayo inadaiwa vyombo vya dola vinatumika kuua na kujeruhi raia.
Wakati jeshi la Polisi nchini likitangaza kuundwa wa timu ya maafisa polisi kupitia timu inayojulikana kama haki jinai, watetezi wa haki za binadamu wamepinga hatua hiyo kwa madai kwamba polisi hawawezi kujichunguza wenyewe.

Nalo Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwa upande wake limelaani kitendo cha kujeruhiwa kiongozi huyo w akikundi cha kiislamu ambaye anadaiwa kutafutwa kutokana na tuhuma za uchochezi baada ya kupewa kifungo cha nje na mahakama moja jijini Dar es salaam.
Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Alhad Mussa Salum amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es salaam kwamba iwapo Polisi mkoani Morogoro wamehusika na kujeruhiwa kwa Sheikh Ponda, basi wamefanya kitendo kibaya ambacho kinaondoa imani ya wananchi kwa jeshi hilo.
Akizungumzia uhusiano wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania na Taasisi inayoongozwa na Sheikh Ponda, ambayo inadaiwa kutotambuliwa, Alhad Mussa amesema Bakwata haina uadui na Sheikh Ponda kiasi cha kumtaka adhurike.
Naye kamanda wa kanda maalum ya kipolisi Dar es salaam Suleiman Kova alithibitisha kujeruhiwa na kulazwa kwa shekhe Ponda katika taasisi ya mifupa MOI jijini Dar es alaam huku akitaka masuala mengine yanayohusiana na kukamatwa kwake kuachiwa kamanda wa polisi mkoani Morogoro.
Akiwa mkoani Morogoro juzi Sheikh Ponda Issa Ponda alijeruhiwa begani na kitu kinachodhaniwa ni risasi wakati Polisi mkoani humo walipokuwa kwenye harakati za kumkamata.
http://www.voaswahili.com
Post a Comment