Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amemteua Bwana Adam H. Mayingu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni
kwa Watumishi wa Umma (PSPF).
Taarifa
iliyotolewa mjini Dar es Salaam jana, Jumanne, Agosti 13, 2013, na
kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa
uteuzi unaanzia Juni 8, mwaka huu, 2013.
Kabla ya uteuzi huo, Bwana Mayingu alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo wa PSPF.
Bwana
Mayingu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa
Mfuko huo, Bibi Hawa Mmanga ambaye amestaafu utumishi wa umma kwa
mujibu wa sheria.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
Post a Comment