Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

‘Kodi zinatishia viwanda nchini’

Tanga. Mbunge wa Tanga Mjini, Omari Nundu amesema kuna hatari ya viwanda vingi vya sasa kushindwa kujiendeshakama Serikali itaendelea kutoza utitiri wa kodi na ushuru.
             
Amesema kwa uzoefu wake, nchi nyingi zenye zina nia ya dhati ya kuendelea kuwalea wafanyabiashara na wenye viwanda wazalendo zinawatoza kodi watu hao wakati viwanda vyao vinapofikia hatua ya kujiendesha.

Alieleza wasiwasi wake huo alipotembelea kiwanda cha maji ya chupa cha Al Hayaa cha jijini Tanga na kupokea malalamiko kutoka kwa Mkurugenzi, Said Mbarouk kwamba ingawa kiwanda ni kichanga, lakini kinatozwa kodi nyingi.

Nundu ambaye kabla ya kuwa mbunge alikuwa akiishi Ulaya kwa miaka mingi alisema, hajawahi kuona katika nchi yoyote duniani ikiwatoza wafanyabiashara wake kodi ya mauzo na siyo faida.

“Tangu Julai 7 mwaka huu, nipo katika ziara ya kutembelea viwanda vya Tanga, nimetembelea vingi lakini nilichobaini ni kuwa hata vinavyojiendesha kwa sasa vinaweza kufungwa siku si nyingi zijazo kutokana na kukabiliwa na mzigo wa gharama za kuviendesha na hii inatokana na utitiri wa kodi zinazotozwa na Serikali,” alisema Nundu.


Alisema tatizo ni kukosekana kwa mfumo wa kuwapa wafanyabiashara na wenye viwanda wazalendo, likizo ya kodi badala yake wanapewa wawekezaji kutoka nje ambao hata wangetozwa kodi ya aina yoyote wangelipa bila tabu.

“Hii inatokana na ukweli kwamba wengi wao huwekeza matawi ya vitegauchumi vilinavyozalisha faida kubwa katika nchi mbalimbali duniani,” alisema mbunge huyo.

“Viwanda vingi hapa Tanga havipo katika hali nzuri hata kama sasa vinazalisha lakini vinaweza kufungwa wakati wowote na tatizo kubwa ni kodi za Serikali zimekuwa nyingi ghafla,” alisema Nundu na kuahidi kuishauri Serikali ili iweze kuangalia athari za utitiri huo wa kodi yake.

Kwa upande wake, Said alisema licha ya kuwa kiwanda hicho cha maji ya chupa bado ni kichanga lakini kimekuwa kikitozwa kodi kubwa kuliko uwezo wake wa uzalishaji.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top