Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI AZINDUA RASMI “DUTY FREE SHOP” YA KISASA GEREZA KARANGA, MOSHI

 


PIC-1Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima(wa pili kulia) akikata utepe kuashilia uzinduzi rasmi wa Duty free shop ya Gereza Kuu Karanga, Moshi jana Agosti 23,   2013(wa kwanza kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja. PIC-2Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi kwa Mgeni rasmi  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima kabla ya kumkaribisha kuzindua rasmi  Duty free shop ya Gereza Kuu Karanga, Moshi jana Agosti 23,  2013. PIC-3Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima( kulia) akiangalia jiwe la msingi mara baada ya uzinduzi rasmi wa Duty free shop ya Gereza Kuu Karanga, Moshi jana Agosti 23,   2013(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja. PIC-5Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima( katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(wa pili kushoto) pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali wa Mkoa wa Kilimanjaro na Wakurugenzi wa
Transit Military Shop  mara baada ya uzinduzi rasmi.
PIC-6Kikundi cha kwaya ya Kina Mama wa Kambi ya Gereza Kuu Karanga Moshi wakitumbuiza   wakati wa hafla ya Uzinduzi rasmi wa Duty free shop ya Gereza Kuu Karanga mbele ya mgeni  rasmi, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima(hayupo pichani). (Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza)
………………………………………………………………………
Na; Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza, Moshi
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima amepongeza kasi ya Utendaji kazi wa Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja  pamoja na Uongozi wote wa Jeshi la Magereza Nchini kwa kutekeleza kwa mafanikio makubwa mpango wa Serikali wa kuwasogezea huduma za bidhaa muhimu na zenye manufaa Maafisa, askari Magereza na familia zao katika maeneo yao ya  kazi hususani huduma za  “Duty free shops”. Mhe. Pereira Silima ameyasema hayo jana wakati wa  uzinduzi rasmi wa Duty free shop ya Gereza Kuu Karanga, Moshi jana Agosti 23,   2013 katika Viwanja vya Gereza Kuu Karanga Moshi ambapo baadhi ya Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Kilimanjaro walihudhuria hafla hiyo.
 
Aliongeza kuwa Serikali iliidhinisha utaratibu wa Maafisa na askari wa Majeshi ya Polisi na Magereza kusogezewa huduma za kuwapatia bidhaa muhimu katika maeneo yao kwa gharama nafuu. “Lengo la Mpango huu ni kuhakikisha kuwa ustawi wa maisha ya Maafisa na Askari wa Majeshi haya kwa kuwapatia bidhaa zenye bei nafuu ili kuwapunguzia ukali wa maisha” alisema Mhe. Silima.

Aidha, Mhe. Silima amewaasa Maafisa na askari watakaotumia huduma husika kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu pamoja na maadili ya uendeshaji wa maduka hayo ili kuhakikisha kuwa adhima ya Serikali ya kuwapunguzia makali ya maisha  Maafisa, askari  pamoja na familia zao wananufaika ipasavyo na si vinginevyo.

Awali akimkaribisha Mgeni rasmi,Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja  alisema kuwa Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Transit Military Shop LTD limeazimia kusambaza huduma za Duty Free Shop nchi nzima kwa ajili ya kutoa huduma kwa Maafisa na askari.

Kamishna Jenerali Minja alimhakikishia Mgeni rasmi kuwa maduka hayo yataendeshwa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taza Duty Free Shop na akasema kuwa hata sita kuchukua hatua kali za kinidhamu kwa Maafisa na askari watakao kwenye kinyume na uendeshaji wa huduma hizo.

Hivi sasa Jeshi la Magereza limefanikiwa kuzindua jumla ya Duty Free Shops tatu(03) katika ya Ukonga, Dar es Salaam, Gereza Isanga Dodoma na Gereza Kuu Karanga, Moshi na tayari maandalizi ya uzinduzi katika Mikoa ya Morogoro, Mwanza, na Mbeya yatakamilika hivi karibuni.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top