Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

POLISI MKOANI KATAVI YABAINI MTANDAO MPYA WA MATAPELI

 


SAM_2469Kibada wakibada, Katavi
POLISI  mkoani Katavi  imeubaini  mtandao  wa matapeli   uliojitanua katika  mkoani  humo  pia katika mikoa  ya Rukwa  na Mwanza  kwa  kuwatia nguvuni  vinara  wake akiwemo  mwanamke mmoja wakituhumiwa  kutapeli  watu  kwa kujifanya  wanatoa huduma  za uganga  wa jadi pasipo  kuwa  na  kibali .
Kamanda wa Polisi mkoani  hapa , Dhahiri Kidavashari  aliwataja   vinara  wa matandao  huo wa kitapeli  kuwa  ni pamoja na Issa Hassan(42) ,Hussein  Hassan  maarufu Rwango (38)  wakiwa wakazi wa jijiji la Mwanza,na Magreth Bakari (45)  mkazi  wa Mtaa wa Nsemlwa  mjini Mpanda  mkoani Katavi Charles  Mwelela (38.)akiwa ni mkazi wa sumbawanga mkoani Rukwa.
 Alibainisha hayo  leo  wakati  akizungumza na  waandishi  wa habari   ofisini  kwake  huku akiwaonesha  watuhumiwa hao  wanne  pia  tunguli  zao wanazodaiwa kuzitumia  kutapeli  wananchi mbalimbali  nchini ambapo  Agosti 26 mwaka  huu , saa  tano  usiku  watuhumiwa hao  walikamatwa  katika Mtaa wa Mji mwema mjini hapa  katika  nyumba ya kulala wageni  iitwayo Vatikani .
Miongoni  mwa  tunguli  hizo alizozioensha kwa  waandishi  wa  habari  na  baadhi ya  maofisa  wa  polisi  ni pamoja na ndege aliyekaushwa  ambaye  hutumika  kwa  kuwafanya  wanaume  watii  kila kitu  wanachoamriwa na wake  zao  ikiwemo  kupika  hadi  kufua nguo  za  wake  zao .

Pia alionesha  uga  mweupe ambao  watuhumiwa  hao  walikuwa  wakitumia kuwalevya   watu  kwa kuwawekea  kwenye vileo  na kuwaibia  fedha  zao  zote  kisha  hutokomea kusikojulikana pia  wamekujwa  wanawatapeli  watu  kwa  kuwadanganya  kuwa  wana pasi  ya Mjerumani  ambayo  ni feki  ambao  inauzwa  kwa zaidi ya  milioni 20  kwa madai kuwa  ina uwezo wa ‘kuzalisha “mabilioni  ya  fedha . .
Kwa mujibu wa Kamanda  huyo  watuhumiwa hao  wanadai  kuhusishwa  na  matukio ya kitapeli  ambapo   baadhi ya wafanyabiashara  kadhaa  wametapeliwa  mamilioni  ya  fedha baada ya  kuwekewa  unga  mweupe  wenye  uwezo  wa  kumlaza  mtu kwa saa  kadhaa kabla  hajazinduka .
“Uchunguzi  wa  awali  wa kipoli  umebai  kuwa  watuhumiwa hawa  hutapeli  wagtu  kwa mtindo  wa kuwapa  madawa ya kulevya  na muda mwingine  huwa  wanawatapeli  watu kuwa  wana   wana pasi  ya Mjerumani  ambayo ni  feki  na kuwataka  watoe  fedha  zao  pasipokujua  kuwa  wanatapeliwa’ alisisitiza Kamanda Kidavashari .
Kwa mujibu wa Kamanda   watuhumiwa  hao  watatu wa kiume  wanadaiwa kukaaa  kwenye vyumba  vya  nyumba  mbalimbali  za  kulala  wageni  wageni  mjini hapa  wakisubiri  wateja wao  huku  mtuhumiwa huyo  wa kike  anakuwepo  nje akitafuta  wateja  kutoka  kona  mbalimbali  za mjini hapa .
“Mwanamek huyo  awapatapo  wateja hao  huwapeleka  kwenye vyumba  walimo  watuhumiwa  wa kiume  kwa ajili ya  kutapeliwa  akijifanya  kuwa  naye   pia ni mteja  kama wao……. Bahati mbaya  sana  kutokana na  jinsia  yake ya kike  ni  rahisi mno  kumuamini  bila kuwa  na hofu naye kwa ni wanawake  wachache wanaojihusisha  katika  matukio ya  kitapeli  mjini  hapa” alisema .
Kwa mujibu  wa Kidavashari  watuhumiwa  hao  wote  wanatarajiwa  kufikishwa  mahakamani  wakati  wowote  mara  tu  uchunguzi  wa awali  wa ksi  yao  utakapokamilika.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top