Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Wataka wafanyabiashara wadogo waondolewe kodi

Photo: Wataka wafanyabiashara wadogo waondolewe kodi

Tanga. Bahweje alisema kodi hiyo imekuwa ikiwaumiza wafanyabiashara wanaochipukia, na kwamba ili waweze kujiinua kiuchumi, Katiba iseme wazi kuwa kodi hiyo haipo.

Alisema kuwepo kwa kodi hiyo kumezidi kuwafanya wafanyabiashara wengi kushindwa kuendeleza biashara zao baada ya kuelemewa na kodi nyingi na hivyo kuitaka Tume hiyo kufuta kipengele hicho.

“Unajua umaskini unasababishwa na Katiba ya sasa, kama kungekuwa hakuna Sheria ya Kodi kwa mfanyabiashara mvuja jasho kila mtu angelikuwa na uhakika wa milo mitatu kwa siku,” alisema na kuongeza

“Hivi kwa nini Serikali haitaki kuondosha umaskini nchini wakati inajua wazi kuwa kodi ndio kikwazo cha kuondokana na umaskini, basi sisi wanyonge mtetezi wetu ni Katika Mpya ijayo tu na ifute kabisa,” alisema Bahweje.

Akizungumzia kuhusu uraia, kiongozi huyo alisema uwepo wa pasi za nchi mbili unaweza kuathiri uhusiano wa nchi na nchi iwapo tu mtu atafanya vitendo vya kihalifu na kuiharibia sifa taifa alilopo.

Alisema ni vyema kuwepo kwa uraia wa nchi moja kitu ambacho kitamuwezesha mtu kuheshimu utaifa wake pamoja na kuutetea utamaduni wa nchi aliyopo, tofauti na kuwa na uraia wa nchi mbili.

Bahweje alisema suala la uraia ni vyema Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya ikalizingatia ili kuweza kulinda utamaduni na rasilimali za nchi kuporwa na watu ambao hawana mapenzi na nchi hii.
Tanga. Bahweje alisema kodi hiyo imekuwa ikiwaumiza wafanyabiashara wanaochipukia, na kwamba ili waweze kujiinua kiuchumi, Katiba iseme wazi kuwa kodi hiyo haipo.

Alisema kuwepo kwa kodi hiyo
kumezidi kuwafanya wafanyabiashara wengi kushindwa kuendeleza biashara zao baada ya kuelemewa na kodi nyingi na hivyo kuitaka Tume hiyo kufuta kipengele hicho.

“Unajua umaskini unasababishwa na Katiba ya sasa, kama kungekuwa hakuna Sheria ya Kodi kwa mfanyabiashara mvuja jasho kila mtu angelikuwa na uhakika wa milo mitatu kwa siku,” alisema na kuongeza

“Hivi kwa nini Serikali haitaki kuondosha umaskini nchini wakati inajua wazi kuwa kodi ndio kikwazo cha kuondokana na umaskini, basi sisi wanyonge mtetezi wetu ni Katika Mpya ijayo tu na ifute kabisa,” alisema Bahweje.

Akizungumzia kuhusu uraia, kiongozi huyo alisema uwepo wa pasi za nchi mbili unaweza kuathiri uhusiano wa nchi na nchi iwapo tu mtu atafanya vitendo vya kihalifu na kuiharibia sifa taifa alilopo.

Alisema ni vyema kuwepo kwa uraia wa nchi moja kitu ambacho kitamuwezesha mtu kuheshimu utaifa wake pamoja na kuutetea utamaduni wa nchi aliyopo, tofauti na kuwa na uraia wa nchi mbili.

Bahweje alisema suala la uraia ni vyema Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya ikalizingatia ili kuweza kulinda utamaduni na rasilimali za nchi kuporwa na watu ambao hawana mapenzi na nchi hii.
 
HABARI LEO
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top