Bharti
Airtel imetangaza leo kwamba michuano ya kimataifa ya vijana chini ya
umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars itaanza kutimua vumbi katika
jiji la Lagos nchini Nigeria kuanzia September 16 hadi 22 ambapo
Tanzania itawakilishwa na timu za wasichana na wavulana.
Michuano
hii inafanyika kwa mara ya pili mfululizo kwa lengo la kutoa fursa kwa
vijana chipukizi kutoka sehemu mbali mbali barani Afrika kuonyesha
vipaji vyao na kuchochea maendeleo ya mpira wa miguu.
Akizungumzia
mashindano hayo Mkurugenzi Mtendani wa Airtel Tanzania Sunil Colaso
amesema: “Michuano ya Afrika ya Airtel Rising Stars itasaidia kuinua
kiwango cha soka barani Afrika na Airtel inafarijika kupata fursa hii ya
kuendeleza vipaji vya wachezaji chipukizi”.
Huu
ni mwaka wa tatu tangu kuanzishwa kwa programu hii ya Airtel Rising
Stars barani Afrika ambapo maelfu ya vijana wamepata nafasi ya kushiriki
katika nchi 16 kuanzia ngazi ya chini, mkoa hadi Taifa.
Wachezaji
nyota kutoka katika kila nchi hizo sasa wanaelekea nchini Nigeria
kuchuana kwa lengo kuonyesha vipaji vyao zaidi na kupata mshindi ambaye
ndiye atakuwa kinara wa Airtel Rising Stars barani Afrika mwaka huu.
Mshindi pia atajinyakulia kitita cha dola za Mimarekani 10,000 ambazo ni
zaidi ya milioni kumi na sita za Tanzania. Fedha hizi zitatumika
kuwaendeleza vijana hao kielimu.
Michuano
hii ya Afrika mwaka jana ilifanyika jijini Nairobi ambapo timu ya
wasichana kutoka Ghana ilinyakua taji huku timu ya wavulana kutoka Niger
ikiukwaa ubingwa kwa upande wa wavulana.
Mchuano
unatarajiwa kuwa mkali zaidi mwaka huu huku timu mwenyeji Nigeria ikiwa
imejianda vilivyo kuhakikisha kwamba wanawapa raha mashabiki wao na
hatimaye kutwaa ubingwa wa mashindano hayo. Timu nyingine zinazotarajiwa
kutoa upinzani mkali na hata kuiadhili Nigeria nyumbani kwao ni Ghana
na Zambia.
Kwa
kuendesha mashindano haya ya vijana Airtel inaelekea kutimiza lengo
lake ililojiwekea awali la kuwa mdhamini mkubwa wa mchezo wa soka kwa
vijana barani Africa.
Wachezaji
bora kutoka katika mashindano hayo ya Afrika watapata fursa ya
kushiriki kliniki mbili zitakazofanyika chini ya usimamizi wa klabu
maarufu duniani: Arsenal na Manchester United. Kliniki hizo zitafanyika
Lagos (Nigeria) na Lubumbashi (Democratic Republic of Congo) mwezi
Aprili 2014 na kusimamiwa na Makocha wa Manchester United na Arsenal.
Akizungumzia
umuhimu ya kliniki za Airtel Rising Stars Colaso amesema: “Zitasaidiwa
kuwaendeleza vijana kisoka na kuwapa hamasa ya kutaka kuwa wachezaji wa
kulipwa”. Kliniki hizo ndizo zitakazozindua rasmi mwaka wa nne mwezi
Aprili 2014.
Awali
kliniki hizo zilipangwa kufanyika baada ya mashindano ya kimataifa
lakini zimelazimika kusongezwa mbele ili kuwa na muda zaidi wa
maandalizi ya kuziboresha.
Credit: Father Kidevu
Post a Comment