
Paroko wa Parokia ya Roho Mtakatifu Cheju Zanzibar, akisaidiwa na Frateri, Richard Haki kupumzika kitandani baada ya kuzungumza na waandishi katika katika Wodi ya Kibasila iliyopo katika Hosipitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijni Dar es Salaam jana.Picha Salim Shao.
DAR ES SALAAM/ZANZIBAR.
PANDRI wa Parokia ya
Mpendae ya Kanisa Katoliki Zanzibar, Anselmo Mwang’amba amesema kuwa
alimwona mtu aliyemwagia tindikali na kumsabab
ishia majeraha na kueleza kuwa anashangaa kuona polisi hawajamkamata hadi sasa.
Akizungumza jana katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili, kwenye Wodi namba 16, Kibasila alipolazwa, Padri
Mwang’amba alisema baada ya kumwagiwa tindikali, alimwona mtu huyo
akikimbia kuelekea katika nyumba moja jirani.
“Kwa kuwa mimi nilikuwa na taharuki na
maumivu, sikuweza kuendelea kumfuatilia, ila dereva aliyenikimbilia
kunipa msaada aliniambia kwamba alimwona mhusika akikatiza kwenye
uchochoro hadi alipoingia kujificha kwenye nyumba iliyopo jirani na eneo
hilo,” alisema.
Alisema majeraha aliyoyapata wakati
akitokea katika duka la huduma za mawasiliano ya mtandao la Shine Shine
saa 10.15 jioni, ambayo yanamsababishia maumivu makali, hayawezi
kumfanya aikimbie Zanzibar, kwa kuwa hata Yesu Kristo wakati alipokuwa
katika kazi za utumishi duniani alipata mateso makali kuliko yake.
“Nilisomea upadri nikiwa Zanzibar
kuanzia mwaka 1976 hadi mwaka 1981 nilipopata upadrisho kamili. Niko
huko kwa kazi ya Mungu wala si mwanadamu, kwa hiyo nikitoka hapa narejea
hukohuko, siogopi, ingawa miaka hiyo nilipokuwa naanza kazi hii
hakukuwa na mambo kama haya,” alisema.
Aliwataka Wakristo wanaoishi Zanzibar
kuendelea kuwa na umoja na upendo pamoja na kuwa makini kwa usalama wao
licha ya matukio magumu yanayowakuta ikiwamo vitisho na kuchomwa moto
kwa makanisa.
Pia aliunga mkono shinikizo la
kutimuliwa kazi kwa Kamishna wa Polisi wa Zanzibar, Mussa Ali Mussa
kutokana na kushindwa kuwakamata watu wanaomwagia watu tindikali.
“Huyu bwana alishindwa hata kunijulia
hali wakati nikiwa hospitali huko Zanzibar, tofauti na nilipokuja Bara
ambako Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema na Kamanda wa Polisi wa
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova walifika kunijulia hali na
kuzungumza nami hospitali.
“Kwa hali hii, naona kwamba tukio langu
ni la kupangwa na litazungumzwa sana lakini baada ya muda
halitashughulikiwa. Atajeruhiwa mwingine tena lakini hatua za dhati za
kudhibiti ukatili huu usiendelee hazijachukuliwa. Mimi ni padri wa tatu
kufanyiwa ukatili,” alisema.
Mapadri wengine ni Ambros Mkenda aliyepigwa risasi na kujeruhiwa wakati Padri Evarist Mushi aliuawa kwa kupigwa risasi.
Al-Shabaab wanaswa Zenji
Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi
Zanzibar limewakamata watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa kikundi cha
kigaidi cha Al-Shabaab cha Somalia. MWANANCHI.


Post a Comment