Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Davis Mosha, DRFA, waipiga Tafu Taswa SC!!

 

MMG22186
Na Mwandishi wetu
Kampuni ya Delina Group na Chama Cha soka cha Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kimeipiga tafu klabu waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa SC) kiasi cha sh milioni 4.2 ili kuwawezesha kushiriki katika mashindano ya wana-habari yaliyopangwa kufanyika Jumapili ijayo mkoani Arusha.
Makabidhiano hayo yalifanyika jana kwenye mgahawa maarufu wa City Sports and Lounge uliopo katikati ya jiji la Dar es Salaam. Katika makabidhiano hayo, mjumbe wa DRFA kupitia vilabu katika mkutano mkuu wa TFF, Benny Kisaka alikabidhi kiasi cha  sh 1.2 huku Mkurugenzi wa kampuni ya Delina ambaye ni mdau mkubwa wa michezo nchini, Davis Mosha alikabidhi shs milioni 3 kwa mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto “Ronaldo De Lima” Omary.
Kisaka alisema kuwa wameamua kutoa msaada huo kutokana na mchango wa waandishi wa habari za michezo nchini kwa mkoa wa Dar es salaam kwani ni wadau wao wakubwa.
“Waandishi wa habari za Michezo wametoa mchango mkubwa wa maendeleo ya michezo nchini, sit u kwa DRFA, bali kwa vyama vyote vya michezo, sisi  DRFA tumekuwa wa kwanza kuonyesha mfano mfano na tunaamini wengine watatuunga mkono ili kufanikisha jambo hili,” alisema Kisaka.
Mosha alisema kuwa amesukumwa sana na  mwamko wa waandishi wa habari ambao wameamua kuonyesha kwa mfano kwa kucheza  soka na mpira wa pete (netiboli).
Alisema kuwa kampuni ya Delina Group imeamua kutoa mchango huo ili kuwawezesha kufanya vizuri katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na kampuni ya Ms Unique kwa kushirikiana na Taswa Arusha na kudhaminiwa na TBL, Tanapa, Mega Trade, Pepsi,  AICC na Wazee Klabu.
 “Huu ni mchango wangu nikiwa kama mdau mkubwa wa michezo, nimefarijika sana na tunaamini kuwa mtafanya vizuri katika mashindano hayo ambapo nimeambiwa Taswa SC ni mabingwa mara mbili mfululizo,” alisema Mosha.
Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary aliwapongeza wadau hao kwa msaada huo mkubwa. “Mbali ya DRFA na Davis Mosha, pia Azam imetupiga tafu safari hii ambapo mbali ya fedha pia wametoa jezi mbili,” alisema Majuto.
Aliwataja wadhamini wengine kuwa ni Bodi ya Ligi (TPL Board) na Kassim Dewji ambao wamechangia kufanikisha ziara hiyo. “Bado tunahitaji msaada  wa hali na mali ili kuweza kufikia bajeti yetu, kwa ajili ya safari hiyo,” alisema Majuto.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top