Mwandishi wa habari Denice Stephano anaripoti kwamba
gari la kubebea wagonjwa limekamatwa likitumika katika wizi ndani ya mgodi wa
Geita na kufanya wapatikane watuhumiwa tisa wa kesi ya wizi wa mafuta katika
mgodi huo wa Dhahabu ( GEITA GOLD MINE ).
Mwendesha mashitaka wa polisi Inspekta Abiner ameiambia
mahakama September 9 2013 kwamba 5/09/2013 saa 7:30 usiku huko eneo la Geita
power ndani ya mgodi wa Geita gold mine watuhumiwa waliiba mafuta lita 630 ya
dizeli, kula njama za kuiba mafuta hayo na kuharibu mali ambayo ni gari la
kubeba wagojwa katika kituo cha Afya cha Nzera kwa kuling’oa
viti...
Mtuhumiwa wa kwanza Hamudi Biemo (28) Dereva wa gari
anatuhumiwa makosa matatu likiwemo la kula njama na kung’oa viti vya
gari.
Abiner ameongeza kuwa washitakiwa hao walitumia gari aina ya Land Crusser yenye namba za usajili T 671 AKW mali ya Halmashauri ya wilaya ya Geita na kuingia mgodini kuiba mafuta aina ya Diesel lita 630 yenye thamani ya Tsh. 1,386,000/= mali ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM)
Waliofikishwa mahakamani ni Hamudi Biembo dereva wa
gari la wagonjwa ,Malemo Paul (31) mkazi wa mtaa wa Mseto Geita,Selemani
Magoso (31 )ambaye ni dereva pikipiki mkazi wa mtaa wa Shilabela Geita, Julias
Boazi (28) mkazi wa Msalala road Geita ). Wengine ni Rashid Hussen (27) -Mlinzi
wa mgodi, Ismail Zuber (26) -mlinzi wa Kampuni ya G4S ,Christoper Kombo
-Operator wa GGM,Joseph Chiristopher (27) -Operator wa
GGM
Wakili wa upande wa utetezi Leonard Bitemo baada ya watuhumiwa kusomewa mashitaka yao na kukana, aliiomba Mahakama ya wilaya kuahirisha kesi hadi wiki tatu ili wateja wake ambao ni Selemani Magoso, Boaz Paul na Milemo Paul wapate nafasi ya kujiandaa kwa ajili ya utetezi....
Madai hayo yalipingwa na mwendesha mashtaka wa poisi
na kuomba mahakama ipange siku za karibu badala ya wiki tatu kwani kuna
mashahidi ambao wanasafiri kwenda nje ya nchi, kesi hiyo itajwe 12/09/2013
ambako watakuwa wamejiandaa na mahakama ilikubaliana na uamuzi huo na
washitakiwa wote (9) wako nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti.











Post a Comment