Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA LEO ACHANJA MBUGA WILAYA YA ITILIMA MKOA MPYA WA SIMIYU

 


1
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akinywa kahawa mara baada ya kukaribishwa na wananchi katika kijiji cha Budalabuhega wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha chama na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi katika wilaya ya Itilima mkoa mpya wa Simiyu leo ambapo amekagua miradi mbalimbali na kuzngumza na wenyeviti wa matawi na mashina katika vikao vya ndani ikiwa ni pamoja na kufungua mashina, kesho ataendelea na ziara yake katika jimbo la Bariadi mjini. PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-ITILIMA SIMIYU 2
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akinywa kahawa huku Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi ndugu Nape Nnauye katikati akimiminiwa kahawa kwenye kikombe katika kijiji cha Budalabuhega.3
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika kijiji cha Budala Budalabuhega leo.
 6
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipita mbele ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kanadi Wilayani Itilima. 7
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua bweni la wasichana katika shule ya sekondari ya Kanadi huku akiongozwa na mkuu wa shule hiyo Mwalimu Samuel George. 8
Hili ni jengo la zahanati ya kijiji cha Nangale kata ya Ndololezi Kinana alikaguikagua pia 10
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozwa na mganga mkuu wa Zahanati ya Nangale Dk. Kerenge Nyawawa wakati alipotembelea na kukagua jengo la zahanati hiyo. 11Mwenyekiti wa kikundi cha wafanyabiashara wa mazao katika kata kijiji cha Mwanihunda Kata ya migato Bw, Michael Ntulugwa akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipokagua ghala hilo la kuhifadhia chakula lililojengwa kwa msaada wa World Vision. 12
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto akiwa amekaa kwenye kigoda wakati alipofika kwenye shina namba 15 Shuleni Kata ya Migato, kulia ni Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi CCM.
14
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana watatu kutoka kushoto aliyekaa akimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Simiyu Ndugu Pascal Mabiti wakati alipokuwa akiongeza na wananchi katika kata ya Migato 15
Wana CCM wa kata ya Migato wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani wakati akizungumza nao katika shina namba 15 shuleni kata ya Migato. 16
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiteta jambo na Mwenyekiti wa wa shina namba 15 Bwana Michael Sama wakati akiwa katika shina hilo kwa ajili ya kuzungumza na wanachama wa shina hilo leo. 17
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza katika mkutano huo.
 18
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea Fedha Taslimu shuilingi 400.000 kutoka kwa Daud Njalu Silanga Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Simiyu wakati alipochangia SACCOS ya Shina namba 15 shuleni Kata ya Migato. 19
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akinywa maji kwa kikombe cha kiasili cha kabila la kisukuma mara baada ya kusimikwa chifu Machibora Kinana 20
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana mwenye mgolole mweusi akijumuika pamoja na Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi  kulia wakishiriki kula chakula cha asili ya kisukuma kinachoitwa Michembe, kutoka kushoto ni mkuu wa mkoa wa Simiyu Pascal Mabiti na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu Dk. Titus Kamani 23
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akihoji jambo kwa Afisa Elimu Wilaya ya Itilima Ndugu Rogers Shimwelekwa wakati alipotembeleaujenzi wa  jengo la halmashauri ya wilaya ya Itilima leo, kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo Dk Leonard Masale na wa pili ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu Dk. Titus Kamani.
 26
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga lipu pamoja na mafundi wakati alipotembelea ujenzi wa jengo la Halmashauri ya wilaya ya Itilima leo 27
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti katika eneo la Halmashauri hiyo. 28
Ndugu Nape Nnauye akipanda mti katika eneo la halmashauri ya Itilima
  30
Mkutano wa ndani ukiendelea chini ya mti. 31
Ndugu Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Gangabilili ambayo ndiyo makao makuu ya Wilaya ya Itilima 32
Umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo leo. 33
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinanaakihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Gangabilili makao makuuu ya wilaya ya Itilima mkoani Simiyu.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top