Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAADHIMISHO YA 16 YA SIKU YA BIMA YAFANA DAR.

 


 Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene (katikati), Kamishna wa Bima, Israel Kamuzora na Mwenyekiti wa Bodi ya Bima, Peter Ilomo (kushoto) wakishangilia wakati wa Maadhimisho ya 16 ya kila mwaka ya  Siku ya Bima nchini jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Benki ya NMB, pamoja na baadhi ya makampuni mengine yalidhamini maadhimisho hayo.
 Mwenyekiti  wa Bodi ya Bima, Peter Ilomo (kushoto), akizungumza wakati wa maadhimidho hayo jijini Dar es Salaam.  Katikati ni Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene na kushoto kwa Naibu Waziri ni Kamishna wa Bima, Israel Kamuzora. Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Benki ya NMB, pamoja na baadhi ya makampuni mengine yalidhamini maadhimisho hayo.
 Kamishna wa Bima, Israel Kamuzora, akiagana na Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene,mara baada ya maadhimisho ya 16 ya kila mwaka ya Siku ya Bima.
 Kamishna wa Bima, Israel Kamuzora (kushoto) akikabidhi nakala ya kitabu kuhusu Elimu ya Bima kwa Jamii kwa mwenye gari, abiria na watembea kwa miguu kwa Sebastian Ndege, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Ndege Insurance, kichozinduliwa wakati wa maadhimisho hayo.
  Wadau wa bima wakiselebuka wakati wa sherehe za maadhimisho ya 16 kila mwaka ya Siku ya Bima jijini Dar es Salaam.
Rais wa Makampuni ya Bima, Maria Mugo akikabidhi tuzo kwa Mkurugenzi wa Masoko wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania, Adelaida Muganyizi wakati wa maadhimisho hayo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top