Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAALIM SEIF AREJEA ZANZIBAR KUTOKA NCHINI INDIA


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis pamoja na viongozi wengine, wakati akiwasili nchini akitokea India kwa uchunguzi wa kawaida wa afya yake.


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na viongozi mbali mbali, wakati akiwasili nchini akitokea India kwa uchunguzi wa kawaida wa afya yake.


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisawapungia mkono wananchi waliojitokeza kumpokea, wakati akiwasili nchini akitokea India kwa uchunguzi wa kawaida wa afya yake.




Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mama Awena Sinani Masoud (kulia), alionesha uso wa bashasha baada ya kuwasili nchini akitokea India. (picha na Salmin Said, OMKR)



Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, leo amewasili nchini akitokea India alikokwenda kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kawaida wa afya yake.



Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar, Maalim Seif alipokelewa na viongozi mbali mbali wa Serikali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdallah Mwinyi Khamis.



Aidha mapokezi hayo ambayo pia yalihudhuriwa na viongozi pamoja na wafuasi wa Chama Cha Wananchi CUF, yaliambatana na shamra shamra mbali mbali za burudani.



Maalim Seif aliondoka nchini tarehe 24 mwezi uliopita kuelekea India kwa ajili ya uchunguzi wa kawaida wa afya yake, utaratibu ambao umekuwa ukifanyika tangu alipofanyiwa upasuaji wa goti miaka mitatu iliyopita.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top