Kufuatia mashambulizi ya kigaidi katika mall ya West
Gate jijini Nairobi, kumekuwepo na uvumi kuhusu mwanamke wa Uingereza aitwaye
Samantha Lewthwaite au ‘White Widow’ kuhusika na tukio hilo. Jana kulikuwa
kumekuwa na picha zilizosambaa katika mitandao ya kijamii pamoja na kuripotiwa
na baadhi ya vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mtandao wa Mail Online wa
Uingereza, za mwanamke ambaye baadhi ya watu waliamini kuwa ni Samantha
Lewthwaite au ‘White Widow’.
Picha ya mwanamke wa Kenya (kushotio) aliyedhaniwa
kuwa ‘White Widow’
Habari iliyokuwa inasambaa ni kuwa mwanamke huyo
aliyedhaniwa kuwa ‘white widow’ alitoroka kwa njia ya kujifanya kumsaidia
mwanamke huyo (kwenye picha hapo juu).
NTV ya Kenya iliamua kusahihisha habari hiyo kwa
kumtafuta mwanamke huyo (kushoto katika picha) na walifanikiwa kumpata na kuweka
taarifa hiyo sawa kwa kukanusha kutokuwa mtu ambaye watu
walimdhania.
Akiongea na NTV Mwanamke huyo alijitambulisha kwa jina
la Henna, na wakati wa tukio alikuwa katika mall ya West gate na wanae wawili
pamoja na dereva wakifanya manunuzi ndipo ghafla mashambulizi yakaanza. Wakati
wa kujiokoa aliamua kuwa msamaria mwema kwa kumsaidia mwathirika mwenzie
aliyejeruhiwa kama ilivyoonekana katika picha iliyozuwa uvumi wa kuwa ‘white
widow’.
Mtazame hapa chini
Post a Comment